banner68
banner58

Ali Kiba awaomba Watanzania kuoa ili kutulia

Ali Kiba awaomba Watanzania kuoa ili kutulia

20 April 2018 Friday 13:02
Ali Kiba awaomba Watanzania kuoa ili kutulia

Na Amini Nyaungo

Ali Kiba amewaomba watu wote waliofika umri wa kuoa huku wana uwezo wa kutunza wenza wao hawana budi kuliendea jambo hilo muhimu katika maisha yao.

Akiongea na Azam TV wakati wa sherehe yake baada ya kuoa hapo jana jijini Mombasa nchini Kenya, amesema maisha ndio haya haya, kama uwezekano wa kuoa upo na mtu unaye na unaweza kumtunza basi oa.

“Ni wakati sahihi kwa aliye na uwezo kuoa ili aweze kupata utulivu, maisha ndio yale yale, kinachotakiwa kupigana na maisha,” amesema.

Msanii huyo wa kizazi kipya anayetamba na kibao chake cha ‘Seduce me’ aliyoitoa Augusti 25, 2017, aliingia ukumbini hapo jana akishangiliwa sana huku baadae akaimba baadhi ya nyimbo zake.

Nyimbo ambazo zilionekana kufurahiwa sana katika ukumbi huo ni ‘Seduce me’ pamoja na ‘Kimasomaso’ ambao ameurudia hapo awali ulitungwa na mkongwe wa muziki kutoka Zanzibar Issa Matona.

Azania Post

Updated: 20.04.2018 13:13
Keywords:
Ali Kiba
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.