banner68
banner58

Ali Kiba azindua kinywaji Mofaya

Kinywaji hicho kimetengenezwa na kampuni kubwa nchini Afrika Kusini na kuanzia leo kitakuwa kinapatikana madukani

Ali Kiba azindua kinywaji Mofaya

Kinywaji hicho kimetengenezwa na kampuni kubwa nchini Afrika Kusini na kuanzia leo kitakuwa kinapatikana madukani

30 April 2018 Monday 11:22
Ali Kiba azindua kinywaji Mofaya

Na Amini Nyaungo

Msanii wa kizazi kipya ‘Bongo Flava’ Ali Kiba ametumia usiku wa jumapili katika harusi yake kuzindua kinywaji kipya kilichotajwa kwa jina la ‘Mofaya.

Ali Kiba alitumia harusi hiyo ambayo ilifanyika usiku wa kuamkia leo Jumatatu katika ukumbi wa Serena Hotel Jijini Dar es Salaam.

Kinywaji hicho cha Mofaya hakina kilevi na kinaongeza nguvu huku kikichangamsha akili wakati ukiwa umechoka alisema Ali Kiba.

“Nina furaha sana, kuona watu wananiunga mkono, nimewaletea kinywaji changu kinaitwa Mofaya, kinywaji ambacho kinakuchangamsha na kukupa nguvu, pia hakina kilevi,” amesema.

Kinywaji hicho kimetengenezwa na kampuni kubwa nchini Afrika Kusini na kuanzia leo, watu wataanza kupata bidhaa hizo kupitia maduka mbalimbali nchini.

Ali Kiba moja ya wasanii walio na mashabiki wengi hapa Tanzania na anafanya vizuri kupitia tungo zake zinazobeba ujumbe kwa jamii.

Msanii huyo ana album mbili pamoja na vibao vingi ambavyo amesema atatengeneza album nyingine kwa ajiri ya mashabiki wake.

Azania Post

Updated: 01.05.2018 16:37
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Paul 2018-05-05 00:00:21

Je alikiba ndie mmiliki harali wa hcho knywaj au ni baloz kwa ukandaa huu afrka maxhariki?