banner68
banner58

Ali Kiba kufunga ndoa usiku wa leo

Inasemekana anafungia huko nchini Kenya, kwa binti wa huko

banner57

Ali Kiba kufunga ndoa usiku wa leo

Inasemekana anafungia huko nchini Kenya, kwa binti wa huko

13 April 2018 Friday 18:05
Ali Kiba kufunga ndoa usiku wa leo

Na Amini Nyaungo

Msanii nyota wa kizazi kipya Ali Kiba anataraja kuoa usiku wa leo baada ya baadhi ya picha za sherehe kuanza kuonekana mitandaoni.

Ukurasa wa Instagram wa Radio Pilipili ya Nchini Kenya umeweka baadhi ya picha huku ujumbe ukiwa unasema, “Maandalizi ya harusi ya Ali kiba yameshika kasi nyumbani kwa mrembo Amina, mke mtarajiwa wa Kiba, eneo la Kongowe katika katika eneo la bunge la Nyali’.

Ali Kiba amekuwa msiri katika mambo yake ya binafsi hadi sasa hakuna upande wa Ali Kiba uliothibitisha habari hizo japo mashabiki wake wamekuwa wakionesha kufurahishwa na tukio hilo la kuoa.

Moja ya mahojiano yetu na Ali Kiba hapo zamani aliwahi kusema kuwa ipo siku ataoa na kuwa mme halali.

Ali Kiba hivi sasa anatakiwa na mashabiki wake kutoa nyimbo mpya baada ya ‘Seduce Me’ kupungua ladha.

Azania Post

Keywords:
Ali Kiba
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.