Ali Kiba na Diamond wakubwa huko duniani

Ali Kiba na Diamond wakubwa huko duniani

30 May 2018 Wednesday 13:37
Ali Kiba na Diamond wakubwa huko duniani

Na Amini Nyaungo

Kundi la muziki kutoka Nigeria Shiikane wamechambua muziki wa Ali Kiba na Diamond barani Afrika na Uingereza.

Shikane wamesema Ali Kiba na Diamond wanafanya vizuri sana kimuziki nje ya Afrika huku wakiwataja kuwa miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri nchini Nigeria pamoja na Vanessa Mdee. Wameweka wazi kwamba nyimbo za wasanii hawa zinapigwa sana nchini Nigeria.

"Ali Kiba tulikutana Uingereza katika tamasha moja ambapo Ali Kiba alifanya vizuri, huku Diamond pia alifanya vizuri maeneo mengine," wamesema.

Kundi hilo ambalo linaundwa na wasichana watatu ndugu likiwa maarufu kwa jina la Shiikane na linafanya shughuli zake nchini Nigeria na Uingereza.

Linaloundwa na wasanii watatu, wawili miongoni wao wakiwa ni mapacha, Princess Annamay, Shayshay na Baby-K.

Wasanii hao wamesema wanatafuta 'collabo' hapa bongo huku wakiangalia zaidi muziki wao kufanya vizuri Tanzania.

Azania Post

Updated: 30.05.2018 13:41
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.