Ali Kiba na Diamond wapeana mikono Leaders Club

Washangiliwa na waombolezaji

Ali Kiba na Diamond wapeana mikono Leaders Club

Washangiliwa na waombolezaji

23 April 2018 Monday 12:55
Ali Kiba na Diamond wapeana mikono Leaders Club

Na Amini Nyaungo

Ibada ya aliyekuwa ‘Video Vixen’ wa Tanzania Agnes Masogange iliyofanyika viwanja vya Leaders Club Kinondoni Dar es Salaam kumewakutanisha wasanii maarufu nchini Ali Kiba na Diamond Platnumz.

Katika tukio hilo Diamond na Ali Kiba walishikana mikono, kitendo kilichovuta hisia za wengi hisia kubwa sana miongoni mwa waombolezaji jana.

Wasanii hao walishikana mikono na badala ya watu kuhani msibani walianza kushangilia tukio hilo.

Wawili hapo ambao wanafanya vizuri katika Sanaa ya muziki wa kizazi kipya maarufu kama ‘Bongo flava’ huku ugomvi wao ukinogeshwa katika mitandao ya kijamii.

Tukio hilo limemvutia hata aliyekuwa anasherehesha shughuli hiyo MC Pilipili ambaye baada ya kuona wanasalimiana akaanza kusema kuwa, “Mnaona hawana tatizo hawa watu.’

Agness amesafirshwa kwao kwa ajili ya mazishi huko Mbeya na baba yake mzazi ameamuru azikwe pembeni mwa nyumba yake.

Azania Post

Updated: 23.04.2018 13:53
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Mbaga 2018-10-24 09:37:33

Mond piga kaz na alikiba tuione mashabk

Avatar
alikiba hela 2019-05-17 13:34:07

alikiba hela