Baada ya kuachwa na Zari, Diamond aanza kukumbwa na mikosi

Baada ya kuachwa na Zari, Diamond aanza kukumbwa na mikosi

14 June 2018 Thursday 14:17
Baada ya kuachwa na Zari, Diamond aanza kukumbwa na mikosi

Na Mwandishi wetu

Inawezekana kuachana na Zari imekuwa kama mkosi kwa msanii nyota wa muziki hapa Tanzania Diamond Platnumz, baada ya dili lake la kutumbuiza katika sherehe za kuanza kwa michuano ya kombe la dunia kuishia njiani.

Watu wenge wamekuwa wanasema kuwa huenda kuachana na Zari kumekuwa na mkosi kwa msanii huyo kukosa dili hilo ambalo lililikuwa kubwa kwake kama alivyofanya katika michuano ya Afrika AFCON, alipata nafasi na alitumbuiza.

Coca cola walikuwa wamemuunganisha Diamond Platnumz wa Tanzania na mwanamuziki nyota wa R&B kutoka nchini Marekani, Jason Derulo katika wimbo wao wa ‘Colors’ ambapo sehemu ya kwanza aliimba Kingreeza na sehemu ya pili ndipo Diamond ameingiza mistari kwa lugha ya Kiswahili.

Wengi walijua kwamba, msanii huyo nyota barani Afrika angeweza kuwa miongoni mwa wawakilishi wa bara hilo kwenye sherehe hizo za ufunguzi wa michuano hiyo mikubwa zaidi ya soka ulimwenguni ambayo inaanza leo, huku kupitia ukurasa wake wa Instagram akisema kuwa atakuwepo siku za nyuma.

Taarifa zilizotoka wiki moja kabla ya kombe la dunia inasema `Live it up` ulioimbwa na Nicky Jam akiwa na mkali wa movie Will Smith pamoja na Era Istrefi ndio watakao tumbwiza leo.

Watatumbuiza katika uwanja wa Luzhniki, kumekuwa na utani mwingi kutoka katika upande wa pili wa timu Kiba wakimtania kukosa kutumbizwa huku wengine wakitaniana wenyewe kwa wenyewe.

Wimbo huo wa Colors ndiyo wa Coca cola ambao ni washirika wakuu wa kombe la dunia ndiyo maana wamejaribu kuwaingiza wasanii hao, Derulo aliwahi kufika Afrika mashariki kushiriki Coke Studio huku Diamond aliwahi kuwa balozi wa kinywaji hicho.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.