Babu Tale amemchana Diamond kwa Hamisa Mobeto

Babu Tale amemchana Diamond kwa Hamisa Mobeto

05 June 2018 Tuesday 15:44
Babu Tale amemchana Diamond kwa Hamisa Mobeto

Na Amini Nyaungo

‘Mzarau mwiba mguu huota tende.’ Huu ni msemo maarufu hasa kwa watu wa pwani ya Afrika Mashariki ambao hasa hutumia lugha ya Kiswahili ikiwa ni onyo kwa mtoto ambaye anakuwa ameelekezwa jambo lakini iwapo atapuuza na kufanya atakayo, basi huenda akakutana na mabaya siku za usoni.

Hayo yamewekwa wazi na Meneja wa Diamond alipokuwa anahojiwa katika kituo cha Wasafi TV, kuwa alimwambia Diamond kama anataka urafiki na Hamisa afanye urafiki wa kawaida hapo zamani kabla hajazaa naye.

“Nikamwambia pia Diamond kama unafanya ujana, inatakiwa pia uangalie ujana wako, Zari amekuzalia mtoto,” Babu Tale alisema.

Maneno yake yamekuja baada ya kutoka Afrika Kusini katika harakati za kumaliza mgogoro wa Zari na Diamond ambapo hata hivyo bado haijawa wazi amefikia wapi katika kufanikisha hilo.

Wachambuzi wa mambo wanasema kelele zote hizo pamoja na kiki wanaifanyia kutengeneza `Reality show` yao ambayo inatolewa wiki hii ikiwa Diamond amethibitisha hapo jana kuwa akirejea `show` yao itafanyika ikiwaonesha familia yake na namna gani wanaishi.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.