Babu Tale kumaliza tofauti ya Zari na Diamond leo

Babu Tale ameyasema haya kupitia ulimwengu wa Instagram

Babu Tale kumaliza tofauti ya Zari na Diamond leo

Babu Tale ameyasema haya kupitia ulimwengu wa Instagram

02 June 2018 Saturday 10:41
Babu Tale kumaliza tofauti ya Zari na Diamond leo

Na Amini Nyaungo

Meneja wa Diamond ambaye pia alikuwa anasimamia Tip Top Connection, Babu Tale amejifunga kibwebwe kurudisha penzi la Zari ‘The boss Lady’ na Nasib Abdul baada ya kusitishwa kwa miezi minne sasa.

Babu Tale jana alitumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea namna atakavyorudisha penzi hilo ambalo kwa maneno yake anaona kama kumsukuma mlevi vile.

Kumbuka Zari aliwahi kufanya mahojiano na shirika la utangazaji la Uingereza la BBC Swahili na kusema kuwa hawezi kurudiana na Diamond licha ya wawili hao kuonekana kuwa bado wanapendana.

Babu Tale ameyasema haya kupitia ulimwengu wa Instagram ambao sasa hivi kwa Watanzania ni kama ndio sehemu yao ya kushinda.

“Naona watu mnaniandikia niwarudishe Mr and Mrs Dangote, hili kwangu ni kama kumsukuma mlevi yani kazi ndogo sana, ila Niliwaacha tu kwanza kila mtu sumu na hasira za mioyo yao ziwaishe ili wakirudiana akili iwakae sawa.

“Sasa naona muda muafaka wa kulitumia jina langu ipaswavyo, kama ambavyo mama Tee ananiita “Godfather”, siendi na magoti wala kutambaa. Nitapanda ndege kwenda hadi SA kuongea na mtu mzima mwenzangu na ninaamini yataisha kwa asilimia 100, wananzengo niende nisiende?”

Huku leo picha zinaonesha katika ukurasa wake wa Instagram amesema yupo tayari kumaliza mgogoro huo na anaonekana yupo Airport kuelekea Afrika Kusini.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.