Dada wa Diamond, Queen Darleen ataka radhi za baba yake

Queen Darlin aliwahi kunukuliwa akisema kuwa, baba yake ni Diamond kwa kuwa anampa kila kitu

Dada wa Diamond, Queen Darleen ataka radhi za baba yake

Queen Darlin aliwahi kunukuliwa akisema kuwa, baba yake ni Diamond kwa kuwa anampa kila kitu

06 June 2018 Wednesday 14:35
Dada wa Diamond, Queen Darleen ataka radhi za baba yake

Na Amini Nyaungo

Msanii wa kizazi kipya Queen Darleen ameomba msamaha kwa baba yake mzee Abdul Juma baada ya kuhitalifiana naye siku za nyuma.

Darleen ambaye ni dada wa Diamond, wakiwa wamechangia baba ambaye ni Abdul Juma, anatamani kumpelekea zawadi mzee huyo baada ya kukorofishana miezi kadhaa iliyopita.

Darleen aliwahi kusema katika moja ya mahojiano yake na waandishi wa habari kuwa baba yake ni Diamond kutokana na huduma mbalimbali anazozitoa huku akisahau kuwa baba yake mzazi yupo licha ya kuwa na hali ya kawaida kimaisha.

Baada ya kusikia hayo Mzee Abdul naye amesema wazi kuwa sio mwanae kama amediriki kusema Diamond baba yake basi yeye sio mwanae tena.

Kwa maneno ya mzee Abdul Juma kwa waswahili wanasema amemtolea radhi.

Leo kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram, Queen Darleen ameandika maneno ambayo yanamlenga mzee huyo kwa ajili ya kumpa zawadi ili mambo yawe sawa.

Ameandika kama fumbo ila chini akasema kabisa akimpa zawadi mzee wake atakubali.

“Usisahau yule aliyekuwa anakununulia nguo za Eid (Baba), msisahau kuwapa zawadi wazazi wenu wawili wakiwa hai na msisahau kuwatolea sadaka na kuwaombea dua wazazi wenu waliotangulia mbele ya haki,” ameandika.

Chini ameandika “Allah sijui kama Mzee Abdul atakubali zawadi yangu,” Darleen aliishia hapo na ndipo watu walipoanza kutoa maoni yao huku wakisema kuwa hakuna mzazi atakayekataa zawadi ya mtoto wake wamemshauri ampe.

Bado watu wanasema kiki zinaendelea kuelekea katika `Reality Show` ya Wasafi ambayo itaonesha maisha ya Diamond na familia yake.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.