Diamond amponza Hamisa Mobeto, ashambuliwa kila kona

Ashutumiwa kuharibu penzi la Diamond na Zari

Diamond amponza Hamisa Mobeto, ashambuliwa kila kona

Ashutumiwa kuharibu penzi la Diamond na Zari

06 June 2018 Wednesday 12:40
Diamond amponza Hamisa Mobeto, ashambuliwa kila kona

Na Amini Nyaungo

Mrembo Hamisa Mobeto amezidi kukabiliwa na wakati mgumu katika mitandao ya kijamii, kutokana na uhusiano wake na staa wa Bongo Flava Diamond Platnumz.

Uhusiano huo umekuwa gumzo katika siku za hivi karibuni, kutokana na Mobeto kukabiliwa na matusi na kashfa kwa kila anachondika.

Kila kona mwanamitindo huyo amekuwa hana furaha tena hadi anafikiria kufuta ukurasa huo wa Instagram wenye wafuataji milioni 2.3.

Hapo jana ameposti video ikionesha viatu ambavyo vinapatikana kupitia duka lake la Mobeto Fashion lililopo jijini Dar es Salaam, na kuwafanya watu kumjia juu na kusema ashukuru kwa kufunguliwa duka na Diamond.

Hata hivyo alilazimika kujibu kwamba, alifungua duka hilo kwa fedha zake mwenyewe na ndiyo maana limechelewa kukamilika.

Baada ya kuona hayo, mama yake mzazi mwanamitindo huyo ambaye anatumia jina la ‘Mama Mobetto’ ameandika mengi ya kuwaomba wanaomtukana mwanae waache mara moja.

“Mmemtukana mwanangu hadi tumbo la uzazi limeniuma natamani ningewazaa wawili, pia ningeomba familia zote zilizopo Instagram mpumzisheni matusi na kumdharilisha mwanangu. Kama kawakosea, ninamuombea msamaha mwezi huu mtukufu. Mpeni amani ili na mimi nipate furaha ya uzazi wangu,” ameandika mama yake.

Baadhi ya watumiaji wa mtandao huo wanamshutumu Mobeto kwa kuingilia penzi la Diamond na mrembo kutoka nchini Uganda Zari, hivyo kuwa sababu ya wawili hao kutengana.

Yote hayo yanatokana na maneno ambayo yapo katika familia ya Diamond kuhusu Hamisa wakati huo huo bado taarifa za kurudiana na Zari bado zinaenda chini chini.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.