banner68
banner58

Diamond azua kizaazaa kuagwa kwa Masogange

Diamond azua kizaazaa kuagwa kwa Masogange

22 April 2018 Sunday 17:22
Diamond azua kizaazaa kuagwa kwa Masogange

Msanii wa Bongo Flava na kiongozi wa kundi la Wasafi ‘WCB’, Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz, amesababisha kizaazaa kwenye viwanja vya Leaders, katika shughuli za kuuaga mwili wa marehemu Agnes Gerald Waya, maarufu kwa jina la Agnes Masogange.

Diamond amesababisha kizaa zaa hicho mara baada ya mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Steven Nyerere, kumkaribisha kwa ajili ya kutoa salamu zake za pole kwa wafiwa na watu wote walikuwa kwenye viwanja hivyo.

Mara baada ya kusikia Diamond anakuja kuzungumza, waandishi wa habari waliokuwa kwenye viwanja hivyo, walianza kuvuruga utaratibu na kutoka sehemu walizokuwa wamepangiwa kueleke sehemu aliyokuwa Diamond.

Mara baada ya kutokea tafrani hiyo, ndipo MC Pilipili, aliyekuwa mshereheshaji wa tukio la kuagwa kwa mwili wa Masogange, kwa kushirikiana na Steven Nyerere, walipowaomba waandishi wa habari hao kurudi sehemu zao za awali, ili shughuli zingine ziweze kuendelea ikiwemo msanii Diamond kutoa salamu zake za pole.

Baada ya maelezo hayo, waandishi wa habari waliweza kurudi kwenye sehemu zao, na hivyo kutoa nafasi kwa Diamond kuweza kuzungumza, ambapo amesema amsesikitishwa sana na kifo cha Masogange, huku akiwasii wasanii wenzake kumkumbuka Mungu katika enzi za uhai wao ili waweze kujitengenezea makao mema mbinguni, endapo safari yao itafika.

“Tupo duniani lakini tunapita, tusijidanganye kwakuwa tunaimba muziki, kamera zinatufuata, watu wanatushangilia, lakini pia tusisahau kuandaa kesho yetu ya tunakoelekea”, amesema Diamond.

DarMpya

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
dazy 2018-04-28 01:36:36

r.i.p masogange i lovd u...god loves u much thus he has taken u to be near him