banner68
banner58

Diamond na Ali Kiba walivyo ipaisha Tanzania kimataifa

Je, unafahamu muziki wa nchi gani unapendwa zaidi Afrika? Soma makala hii

Diamond na Ali Kiba walivyo ipaisha Tanzania kimataifa

Je, unafahamu muziki wa nchi gani unapendwa zaidi Afrika? Soma makala hii

12 June 2018 Tuesday 11:54
Diamond na Ali Kiba walivyo ipaisha Tanzania kimataifa

Na Amini Nyaungo

Muziki wa Tanzania umekuwa kwa kasi sana kwa kipindi cha miaka 10 kutokea 2008 hadi 2018, wakati huo muziki ambao ulikuwa unasikika zaidi ni ule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika kusini, Mali pamoja na Nigeria.

Miaka ya nyuma Tanzania haikuwa katika ramani kabisa licha ya wasanii kutoa ngoma kali na zenye ujumbe, imefika mahali hadi Kenya walikuwa juu ya Tanzania kwa muziki yaani ukizungumzia 10 bora Kenya ilikuwepo.

Afrika Kusini

Wakati huo nakumbuka katika zile tano bora ilikuwa Afrika Kusini wasanii wake wakipiga ngoma aina ya `kwaito` huku Raggae iliyokuwa inashikiliwa na hayati Lucky Dude ikizidi kuinogesha Afrika Kusini bila kuwasahau Branda Fassie, Yvonne Machaka `Chaka chaka` na Mafikizolo.

Muziki wao ulikuwa juu sana na hata Watanzania walifurahi kuucheza muziki wao hadi katika maharusi na sehemu za burudani.

Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo

Jamhuri ya Kongo, ngoma zao zilikuwa hazijifichi wasanii kama Papa Wemba, Tabu Ley, Franco Luambo, Koffi Olomide, Madilu Systim na wengine ambao walifanya vizuri sana.

Watu wengi walikuwa wanacheza na kuimba kwa Tanzania ndio muziki uliokuwa umeshika sana ukiachana Afrika nzima, ilipata mashabiki wengi wakiwa wanachagua wanamuziki wao.

Mali

Nchini nyingine Mali ambapo msanii kama Salif Keita ameweza kufanya vizuri na ameitambulisha vizuri nchi yake na ilikuwa ndio namba tatu.

Wasanii wengine kama vile Ali Farka Touré, Toumani Diabaté, Vieux Farka Touré, Oumou Sangaré, Abdoulaye Diabaté na Khaira Arby wameweza kufanya vizuri katika nchi ya Mali.

Nigeria

Nigeria ndio walikuwa namba nne wao walichokuwa wanawaacha Watanzania ni kuimba kwa lugha ya Kiingereza.

Na kwa faida ya msomaji, taifa hilo la Afrika Magharibi ndiyo taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watu miongoni mwa mataifa kusini mwa jangwa la Sahara. Watu wake wanakaribia milioni 180 sasa, hivyo kuwa chanzo kizuri sana kama soko la muziki kwa wasanii wake na msingi mzuri kwa ajili ya kuuza muziki wa taifa hilo nje ya mipaka ya Nigeria.

Ngoma zao zilikuwa za kawaida ila walipatia katika video kali kuwafanya hadi wengi kuwafahamu na kuwika kimataifa, msanii kama `Two face Idibia` japo wa miaka ya hivi karibuni ila ngoma yake ile `African Queen` ilifanya vizuri sana na kuanza kuutangaza muziki wa nchi hiyo kimataifa.

Wasanii wengine kutoka nchini Nigeria kama Femi Kuti, King Sunny Adé, Chief Stephen Osita Osadebe na Majek Fashek wataendelea kuwa na majina makubwa sana katika muziki Afrika na kimataifa.

Baada ya hao wakubwa wa miaka ya nyuma, majina mengine makubwa yaliibuka na kupata umaarufu mkubwa sana ndani na nje ya mipaka ya Nigeria.

Lakini usisahau kundi la P-Square ambalo kabla halijavunjika ndio ilikuwa kama nembo ya Nigeria, wabongo hawakujua wapi wanaweza kuwashika.

Ghana

Nchini Ghana ilikuwa kulikuwa na wanamuziki kama vile Ebo Taylor, Ben Brako, C. K. Mann na Amakye Dede.

Tanzania imefikaje kuwa namba mbili?

Baada ya kugundua kuwa muziki unahitaji uwekezaji, kuanzia katika video na Audio, pamoja na kujitambua kuwa wewe ni msanii imekuwa sababu tosha ya kuipeleka Tanzania katika nafasi mbili bora za juu barani Afrika.

Diamond amefanyaje?

Mwaka 2013 ndio ulikuwa mwaka ambao muziki umeanza kujitathimini kupitia video yake ya `My Number one` na ndipo akampata Davido akatoa `My Namber One Remix` ikawa tiketi ya muziki wake na yeye kwenda kimataifa

Alifanya video kali akaweza kujitengenezea ufalme wake na kuweza kutusua kimataifa maana baada ya hapo ndipo akaendelea na kutoa vitu vikubwa.

Wakati huo huo Diamond akaweza kutumia jina lake kuweza kujitangaza hata katika skendo mbaya ili azungunziwe kwa siku nzima hapa Tanzania, na ameweza ikamuweka juu hadi leo.

Ali Kiba amefanyaje?

Mwaka 2008 alipata shavu la kurekodi project ya One8 aliyokuwa na Robert Kelly (R. Kelly), mastaa wengine kama vile Two face Idibia kutoka Nigeria, Amani kutoka Kenya, Navio wa Uganda, Fally Ipupa kutoka nchini DRC na wasanii wengine kutoka nchini Namibia.

Alisimama kuanzia 2011 hadi 2014 baada ya kurudi akaungana na Diamond kuipeperusha bendera katika kurekodi ngoma kali pamoja na Video kali.

Upinzani wa Ali Kiba na Diamond

Inawezekana wengi hawajui namna gani upinzani wao unaliamsha dude hasa kuwa na timu mbili ambazo zinakinzana lengo kulenga kibiashara na kusongesha mbele muziki.

Bifu lao lina maana kubwa sana ukianzia viewers katika Youtube pindi ngoma ya msanii itakapotoka, wanatambiana nani amewahi kufika milioni, huku wakimsema endapo mmoja wapo amefanya vibaya katika video.

Kuingia kwa Vanessa Mdee naye mmoja ya watu wanaowafuatilia kwa nyuma Ali Kiba na Diamond huku Rosa REE akifanya vizuri.

Wasanii wengine

Licha ya Diamond na Ali Kiba kuweza kufanya vizuri kimataifa bado wengine wanafanya vizuri na kukimbiza kulisaka soko la kimataifa, Ray Vany mmoja ambaye alichukua tuzo ya BET kwa mara ya kwanza kipingele cha Afrika.

Harmonize naye anafanya vizuri katika gurudumu hilo hivi sasa kutengeneza video yenye thamani ya milioni 20 ni kitu cha kawaida sana ndio maendeleo na hadi sasa baada ya Nigeria ni bongo kimuziki.

Msimamo ukoje

Kwa mujibu wa mitandao ya burudani ya Afrika katika nchi mbalimbali barani Afrika inaonesha kuwa Tanzania iko nafasi ya pili hadi ya Tatu kimuziki.

Moja inakamatwa na Nigeria ambapo kuna wasanii zaidi ya milioni moja, mbili hukamatwa na Tazania wakipokeana na Afrika Kusini ambapo nao wanafanya vizuri hasa wanatu wa Hip Hop.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.