Familia ya Diamond yagawanyika Kuhusu Wema na Zari

Familia ya Diamond yagawanyika Kuhusu Wema na Zari

01 June 2018 Friday 15:19
Familia ya Diamond yagawanyika Kuhusu Wema na Zari

Na Mwandishi Wetu

Wema Sepetu amependa sifa ‘kedekede’ ambazo mama yake msanii Diamond Platnumz amemwaga kwa mama wa wajukuu wake, Zari The Boss Lady.

Hatua hiyo ya Wema, ambaye penzi lake na Diamond liliweka historia ya kuwa gumzo kwenye kiwanda cha burudani nchini, imekuja baada ya Bi. Sandra kuweka picha ya Zari kwenye mtandao wa Instagram na kumsifu kuwa ni mwanamke msafi, akinukuu mistari ya wimbo wa ‘Iyena’ ambao mrembo huyo kutoka Uganda ameng’arisha video yake.

“Mama Latiffah mwenye … #IYENA yake Mwanamke usafi gaga kulisugua Mume akirudi sharti viatu kumvua… @diamondplatnumz ft @rayvanny.”

Wema na Esma walikuwa miongoni mwa waliopenda (Like) picha hiyo na ujumbe huo.

Hata hivyo, baada ya Wema kuipenda picha hiyo, Esma ambaye ni dada yake Diamond aligawanya sifa nyingine kwa Wema hali iliyomvuta naye kusema yake ya moyoni.

Kama ulikuwa hujui, Esma amekujuza kuwa kwenye familia ya Diamond Wema ndiye mbabe wa mapishi.

“Hee kwenye USAFI SASA mama TEE NAMPONGEZA wallah dada msafi huyu kwenye mapishi @wemasepetu unanikomeshaga,” aliandika Esma.

Wema alimjibu wifi yake wanaitana ‘wifi daima’ (Forever Wiii), “Yaani basi hapo ushamiss mahanjumati… Ngoja nirudi nije nikupikie kipenzi changu…”

Hata hivyo, mitandoa ya kijamii imeibuka na hisia nyingi za sifa hizi na jinsi familia na marafiki wa Diamond walivyoibuka kudai wanammisi Zari baada ya kuachia video ya Iyena inayoonesha tukio la ndoa. Wengi wakitamani ingekuwa ndoa kweli!

Kwa mtazamo mwingine, ni kama imekoreza mkanganyiko wa mahusiano kati ya familia ya Diamond na mpenzi wa sasa, mama mtoto wake pia, mrembo Hamisa Mobeto ambaye anadaiwa kukutana na ‘kipondo’ kutoka kwa Tyson Bi. Sandra huko ikulu ndogo ya Madale.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
maria mkinga 2018-10-06 23:11:39

hongora wema sepetu

Avatar
Sule 2018-11-14 12:57:25

Ndoo hiyo kali