Hamisa aibariki ndoa ya Diamond na Zari

Hamisa aibariki ndoa ya Diamond na Zari

02 June 2018 Saturday 18:12
Hamisa aibariki ndoa ya Diamond na Zari

Mwanamitindo Hamisa Mobetto ambaye ni mama wa mtoto wa Diamond Platinumz amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram juu ya baba mtoto wake, Diamond Platinumz mara baada ndugu wa msanii huyo kuongea maneno yaliyoonesha kumkejeli.

Kufuatia maneno hayo ambayo yamezagaa katika mtandao wa Instagram, Hamisa ameibuka na kuandika waraka mzito akimtaka Diamond Platnumz kuoa mwanamke ambaye ndugu, meneja na mashabiki wa Diamond wanamtaka aoe kwani katika andiko lake ameonesha kukerwa na baadhi ya maneno yaliyoongelewa katika mitandao ya kijamii kuhusu yeye mara baada ya wimbo wa Iyena kutoka.

Katika wimbo huo, Diamond ameonekana akifunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake na mama watoto wake Zarinah Hassan.

”Ndo uoe huyo mwanamke ambae anatakiwa na ndugu na manager zako bila kusahau mashabiki, sio kutwa mie mtoto wa watu naandamwa na kukaliwa mie kooni! Sijakuita wala kukufunga kamba, kila siku maneno mimi kwani alishindwa kukufuata kukushauri mpaka akimbilie kwenye matv na mitandaoni?” alifunguka Hamisa.

Mobeto ameweka hayo hadharani baada ya post mbalimbali zilizokuwa zikitumwa na watu wa karibu wa Diamond Platnumz wakidai kuwa wamemkumbuka sana Zari hivyo wanataka arudi ili ndoa iweze kufungukika.

Wimbo wa Iyena pamoja na mistari yake, umewaibua watu wengi na mashabiki wengi ambao wameonekana kumshambulia kwa maneno mwanadada Hamisa Mobetto.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.