Hamisa auambia umma kuwa anaona kiza mbele yake

Hamisa auambia umma kuwa anaona kiza mbele yake

05 June 2018 Tuesday 19:05
Hamisa auambia umma kuwa anaona kiza mbele yake

Na Mwandishi wetu

Huenda wengi wanaodhani Hamisa anajua kiki zinazoendelea kwa Diamond na familia yake watakuwa wamemkosea baada ya mwanamitindo huyo kuandika maneno mazito katika ukurasa wake wa SnapChat anavyojisikia karaha kwa yanayoendelea hivi sasa.

Hamisa ambaye amezaa na Diamond Platinumz mtoto mmoja, bado hajatulia akisema kuwa hajafika pale anapopataka. Wachambuzi wa mambo wakihisi kuoelewa na Diamond huenda ikawa sio njia sahihi.

“Bado sijafika Mwenyezi Mungu aliponipangia na kama mnavyoona barabara yangu ni mbovu, ina mashimo, mabonde na pia matope mengi kwa hiyo safari yangu inakuwa ngumu kidogo.

“Lakini nina imani sana na Mwenyezi Mungu aliyenileta kwenye dunia hii. Nina imani ipo siku nitafika na nina imani barabara yangu hii ni mbovu ipo siku ataisawazisha na kuiweka rasmi.

“Ninakushukuru sana Mungu, nina imani kuna vibaya vingi umeniepusha navyo na pia naimani kuna vikubwa vizuri vyaja. Na nina imani hivi vyote visingenipata mimi kama ningekuwa sina u-special wowote ndani yangu,” hayo ni maneno ya Hamisa kupitia ukurasa wake wa Snap Chat.

Huenda yote yanayoendelea baada ya `Reality show` ya Diamond ndio itafahamika mbivu na mbichi ipi, kama mtu gani Diamond atamuoa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.