banner68
banner58

Harmonize ft Wizkid inakuja?

Harmonize ft Wizkid inakuja?

11 June 2018 Monday 13:36
Harmonize ft Wizkid inakuja?

Na Amini Nyaungo

Baada ya Harmonize na Wizkid kuonekana wakiwa katika video ya pamoja mashabiki wake wameanza kumjia juu.

`Story` ambayo ina uzito mkubwa katika mitandao ya jamii ni Harmonize, amabpo `fans` wake wameonekana kuhitaji kolabo na Wizkid huku wakimtaka afanye haraka ili azidi kuipaisha Tanzania kimataifa.

Masahiki hao wameandika kuwa “fanya haraka ipige kolabo hiyo tupae kimataifa,” moja ya shabiki wake akiandika Instagram.

Juhudu zinazofanywa na wasanii wa WCB kila fursa wanahitaji kuitumia huenda ikazaa matunda kwani moja ya kazi nzuri ni kujituma.

Harmonize ameanza safari yake na wimbo unaofahamika kama `Aiyola` wakati huo akiwa ndiyo msanii wa kwanza kusainiwa na Dimond. Baadae akafanya kolabo ya kwanza na Diamond kabla ya `Bado`.

Kwa sasa Harmonize ni miongoni mwa wasanii wa Bongo wanaofanya kolabo nyingi sana na wasanii wakubwa Afrika.

Hata kolabo yake na Diamond Platnumz ‘Kwa Ngwaru’ alipanga kufanya na Davido.

Kwa kipindi cha miaka miwili Harmonize ameweza kufanya kolabo na wasanii kama Marina kutoka Rwanda, Yemi Alade kutoka Nigeria, Eddy Kenzo kutoka Uganda, Emma Nyra kutoka Nigeria, Willy Paul kutoka Kenya, IYO kutoka Nigeria na OmoAkin kutoka Nigeria.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
mike ngetich 2018-11-03 23:43:14

hapo itakua sawa..

Avatar
ally tiago tz 2018-11-06 19:40:59

kiujumla nawakubari sana WCB kwakazi wanazo fanya
hakika wanafanya mziki kazi Kama kazi nyingine
nawanaipenda kazi yao. Nawashauli wasanii wengine wajiunge WCB hakika mtatoka
Nawaambia hiv ukiingia WCB au ukijiunga na WCB
na ukaimba nawasanii wawili wa WCB umetoka kimzi yaaanii umetisua join now

Avatar
ally tiago tz 2018-11-06 19:42:06

kiujumla nawakubari sana WCB kwakazi wanazo fanya
hakika wanafanya mziki kazi Kama kazi nyingine
nawanaipenda kazi yao. Nawashauli wasanii wengine wajiunge WCB hakika mtatoka
Nawaambia hiv ukiingia WCB au ukijiunga na WCB
na ukaimba nawasanii wawili wa WCB umetoka kimziki yaaanii umetisua join now