Iyena ya Diamond yashindwa kuvunja rekodi ya Hallelujah

Iyena ya Diamond yashindwa kuvunja rekodi ya Hallelujah

02 June 2018 Saturday 11:57
Iyena ya Diamond yashindwa kuvunja rekodi ya Hallelujah

Na Amini Nyaungo

Waswahili wanasema kuimba kupokezana, ni wazi kwamba Diamond Platnumz na Ali Kiba ndio vinara wa muziki wa Tanzania kimataifa kwa sasa.

Baada ya Ali Kiba kutoa `Mvumo wa Radi’ ambao uliweza kushika namba moja katika mtandao wa Youtube kwa wiki mbili mfululizo, sasa Diamond tangu atoe Video ya ‘Iyena’ bado inashika namba moja hadi sasa.

Bado Diamond Platnumz anafanya vizuri kwa idadi ya watazamaji wa video hiyo, japo hajaweza kuvunja rekodi yake ya mwaka jana, ambayo mpaka sasa anaishikilia.

Baada ya kutoka ngoma yake `Iyena` aliyomshirikisha RayVany ambayo ipo katika albumu yake ya ‘A boy ‘From Tandale’ imeweza kufikisha watazamaji milioni moja ndani ya masaa 19.

Rekodi hii imeonekana kushindwa kuivunja ile ya mwaka jana, ambayo alihitaji masaa 15 tu kuweza kufikia idadi hiyo ya watazamaji kupitia wimbo wake wa `Hallelujah` ambao alimshirikisha mwanamuziki wa reagae kutoka nchini Jamaica Morgan Herritage.

Video hiyo hakuiweka katika mtandao wa VEVO kama wanavyofanya mastaa wengine ila ameweka katika Youtube yake ambayo pia ina ‘subscriber’ milioni moja.

Wasanii wengine waliowahi kufanya hivyo ni Wizkid wa kutola nchini Nigeria kwa ngoma aliyomshirikisha mwanamuziki wa Hip Hop Drake kutoka Marekani iliyopata watazamaji milioni moja kwa masaa 22 ila katika mtandao wa VEVO.

Ali Kiba alifuata rekodi hiyo ya watazamaji milioni moja kwa masaa 36 kupitia ngoma yake ya ‘Seduce Me’ kupitia VEVO ambapo alisimama mwenyewe bila kumshirikisha msanii yoyote.

Azania Post

Updated: 02.06.2018 12:10
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.