Kanye West ampa ulaji Burna Boy kwa hili

Kanye West ampa ulaji Burna Boy kwa hili

06 June 2018 Wednesday 16:55
Kanye West ampa ulaji Burna Boy kwa hili

Jina la album mpya ya Kanye West “Ye” linafanana na jina la ngoma ya Burna Boy “Ye” na hivyo tangu Kanye ameachia album mpya, mauzo ya ngoma ya Burna Boy yamepanda kwa kiasi kikubwa.

Mashabiki wengi ambao wanaingia kwenye mitandao kuisikiliza album ya Kanye wamejikuta wakisiliza ngoma ya Burna Boy ambayo ina jina hilo hilo, huku mmoja wa shabiki mmoja akiweka wazi kwamba, baada ya kukosea na kuisikiliza ngoma ya Burna alijikuta akisikiliza album nzima ya Burna Boy.

Burna Boy alitweet video akicheza ngoma ya Kanye na kuandika “Many Thanks Kanye West, Thank Ye, Numbers Up 200%”

Ye ipo kwenye album ya Burna Boy “Outside” iliyotoka mapema mwaka huu.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.