Kauli ya Davido yaleta utata kwa Ali Kiba

Yachukuliwa kama dharau kwa msanii huyo wa Bongo Flava

Kauli ya Davido yaleta utata kwa Ali Kiba

Yachukuliwa kama dharau kwa msanii huyo wa Bongo Flava

17 June 2018 Sunday 11:25
Kauli ya Davido yaleta utata kwa Ali Kiba

Na Amini Nyaungo

Kauli ya Davido imeleta maswali mengi kwa mashabiki wa msanii nyota wa Tanzania, Ali Kiba baada ya nyota huyo kutoka Nigeria, kusema kuwa endapo mkali wa ‘Seduce me’ atamfuata kufanya collabo watafanya bila wasi wasi.

Davido ambaye alifanya ‘show’ kali hapo jana katika ukumbi mpya wa Next Door, kabla ya show alikuwa Clouds FM akitanabaisha kuwa hajafanya bado collabo na Kiba ila ikitokea atafanya wala hakuna tatizo.

Amesema waliwahi kukutana katika show mbili ila bado hawajakaa na kufanya jambo.

“Bado sijafanya kolabo na Ali Kiba ila tayari tushakutana kwenye show kama mbili hivi na ikitokea akija na kutaka kufanya kolabo na mimi basi tutafanya” amesema Davido.

Kauli hiyo ya kama Kiba yupo tayari amfuate ndiye imezua gumzo mitandaoni, wengi wakisema namna wanavyomfahamu Ali Kiba hana muda na mtu tena kwa kauli hiyo kama ni kama ya dharau kwa Kiba, ikiwa inamaanisha kuwa msanii huyo wa Bongo Flava ndiyo anayepaswa kumfuata iwapo atahitaji kufanya nae kitu.

Kila mmoja anaposti kibonzo kinachoonesha Kiba hatomfuata Davido kufanya collabo, bali ataendelea na kazi zake kama kawaida.

Jibu la Davido halina tofauti na lile alilotoa Ali Kiba July 2017 kuhusu kolabo yao.

Alikiba alisema; “Unajua wasanii muda mwingine tunakuwa na maneno ya kuridhisha watu lakini hakijafanyika chochote ila plan zipo, muda tukiupata tutafanya ila sijajua ni lini.”

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
kuc vichi 2018-10-09 19:05:49

davido ni msanii wakawaida 2.ilanivizuli wakifanya collabo