Kauli ya kibaguzi ya Kanye West yaipaishia Album yake

Kauli ya kibaguzi ya Kanye West yaipaishia Album yake

05 June 2018 Tuesday 13:02
Kauli ya kibaguzi ya Kanye West yaipaishia Album yake

Na Mwandishi wetu

Licha ya rapa wa Marekani Kanye West ambaye wiki mbili zilizopita alitoa maneno ya kashfa dhidi ya watu weusi nchini humo akisema kuwa wamejitakia kuwa watumwa.

Kauli yake imeonekana kuwagusa wengi wakiwemo T.I na wengine kumshambulia kwa kauli hiyo, lengo lake kubusti Album yake ambayo inafanya vizuri hivi sasa katika `Platform` mbalimbali mtandaoni.

Namba kamwe huwa hazidanganyi, na namba za Album mpya ya Kanye West “Ye” zinapendeza, kwa mujibu wa TMZ album yake mpya imesikilizwa zaidi ya mara Million 100 ndani ya siku tatu tu tangu imetoka.

Album hiyo ya nyimbo 7 inashika namba moja kwenye chati tangu imetoka kwenye mitandao ya kusikiliza (streaming) ya Spotify na Apple Music, na jumla ya idadi ya wasikilizaji kwenye mitandao yote imefikia zaidi ya mara Million 100

Album ya Kanye pia ilikuwa namba moja kwenye nchi 63 kupitia mtandao wa iTunes, Pia ilikiwa namba moja kwenye Spotify na namba moja kwenye nchi 83 kupitia mtandao wa Apple Music.

Wengi wanamshambulia msanii nyota wa Tanzania Diamond kwa kufanya kiki lakini kiki za Diamond haichafui jamii ya Afrika bali anafanya kwa namna anavyojua mwenyewe.

Unahisi nini kimefanya Album ya Kanye West kufanikiwa/ kusikilizwa sana?

Je kauli yake ya kuwakashifu watu weusi pamoja na ukweli kwamba, yeye pia ni mweusi kumefanikisha albamu yake hiyo? Ingia katika mitandao yetu ya kijamii facebook, Instagram na Twitter kwa maoni yako.

Azania Post

Keywords:
Kanye West
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.