banner68
banner58

Kumbe Diamond anapenda Simba: Manara kumpigia magoti afanye wimbo wa Simba

Kumbe Diamond anapenda Simba: Manara kumpigia magoti afanye wimbo wa Simba

12 June 2018 Tuesday 12:05
Kumbe Diamond anapenda Simba: Manara kumpigia magoti afanye wimbo wa Simba

Na Amini Nyaungo

Msemaji mkuu wa Simba Haji Manara anafikiria kumpa kazi Diamond Platnumz ya kutunga wimbo mahsusi kwa ajili ya klabu ya Simba.

Hii imekuja baada ya msanii huyo kujificha kwa muda mrefu hatimaye hapo jana katika utoaji tuzo kwa muwekezaji mkuu wa Simba Mohamed Dewj amethibitisha kuwa yeye ni shabiki lialia wa Simba.

Diamond amesema wazi kuwa hawezi kujiita Simba kisha akashabikia Chui, lazima jina la Simba liendane na ushabiki wake kwa klabu hiyo.

Msanii huyo ameonekana kushindwa kuwataja japo wachezaji wawili wa Simba ambao anawapenda zaidi, tofuati na mwenzake Ali Kiba aliwahi kusema anapenda soka la Ibrahim Ajibu.

“Siku zote unajua siwaambiagi watu mimi ni timu gani, mimi ni Simba. Mimi siwezi kujiita Simba nikashabikia Chui. Mimi ni Simba na Timu yangu ni Simba ndio maana leo nipo hapa,” Diamond alisema.

Baada ya maelezo hayo Msemaji wa Simba Haji Manara ameandika maneno kama ya kijembe hivi kuwa Diamond ni msanii mkubwa Afrika kama unabisha basi kabishie kwenu, huku akisema kuwa akimaliza kuweka mambo sawa atamfuata msanii huyo ili watengeneze ngoma kwa ajili ya klabu hiyo, na haya ndio maneno yake.

”Wewe huwezi kujiita Simba kisha ukashabikia naniliu, huyu ni msanii mkubwa Africa, ubishi nipelekee kwenu kajificha lakini mwisho kaweka wazi, unajua kwa nini? ni kuset standard za brand na ndio nafanya hapa Simba Sc, na soon tutamuomba afanye dude heavy la Mnyama.”

Kuwa na wimbo wa klabu sio kitu kigeni duniani lakini kwa Afrika imekuwa adimu sana kuweza kuona klabu ina wimbo wake maalumu.

Yanga walijaribu kuifanya hivyo na walisema iko tayari miezi minne iliyopita hakuna kinachoendelea hivi sana.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.