Laiza aliwahi kufanya kazi na Ali Kiba

Laiza aliwahi kufanya kazi na Ali Kiba

13 June 2018 Wednesday 13:31
Laiza aliwahi kufanya kazi na Ali Kiba

Na Amini Nyaungo

Mtayarishaji wa muziki ‘producer’ wa label ya Wasafi Classic Baby, Laiza amesema yeye ni miongoni mwa watu waliofanya kazi na wasanii wakubwa Afrika mmoja wao ni Ali Kiba.

Amesema Ali Kiba aliwahi kufanya naye kazi kabla ya kujiunga na Wasafi Classic Baby (WCB) wakati huo huo alifanya kazi na Ice Prince wa Nigeria, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpozy’ pamoja na hayati Sharo Milionea.

“Hawa wote nimepata bahati ya kufanya nao kazi kwa kiwango cha hali ya juu, hii inaonesha namna gani nimekuwa na bahati ya kufanya kazi na watu hao,” amesema.

Laiza ni moja ya watayarishaji wa muziki hapa Tanzania wanaofanya vizuri katika midundo kupitia label yake hiyo.

Miongoni mwa ngoma ambazo amezitengeneza ni pamoja na Kokoro ya Rich Mavoko, Kwa Ngwaru ya Harmonize, Eneka ya Diamond, Bora Tuachane ya Lava Lava, Kwetu ya Rayvanny, Kijuso ya Queen Darleen, na Bado Harmonize akimshirikisha Diamond.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.