Mara ‘pap Diamond’ aibuka katika show ya Clouds

Ni baada ya kuwa na mvutano wa muda mrefu na uongozi wa redio na televisheni ya Clouds

Mara ‘pap Diamond’ aibuka katika show ya Clouds

Ni baada ya kuwa na mvutano wa muda mrefu na uongozi wa redio na televisheni ya Clouds

17 June 2018 Sunday 11:37
Mara ‘pap Diamond’ aibuka katika show ya Clouds

Na Amini Nyaungo

Mambo ya burudani huwa hayajifichi, siku za kati kulikuwa simtofahamu kati ya uongozi wa Clouds na msanii Diamond Platnumz.

Kumekuwa na mgogoro wa chini kwa chini baina ya Diamond na uongozi wa Clouds Media, huku mashabiki wa muziki nchini wakiachwa na sintofahamu. Ngoma za msanii huyo maarufu barani Afrika ni kama zimepigwa marufuku kusikika ndani ya redio ama kuonekana katika televisheni inayomilikiwa na Clouds Media.

Mara kadhaa, msanii huyo amekuwa akisikika akitoa vijembe dhidi ya redio na televisheni hiyo maarufu nchini.

Ukiuliza urafiki wao umeisha vipi hakuna anayejibu sawa sawa, ndio maana Edwini Senzaba amesema mambo ya ‘Ngoswe muachie Ngoswe’.

Jana Next Door imetokea nini?

Mchongo uko hivi, Davido alikuwa na show hapo ambapo imeandaliwa na Uongozi wa Clouds.

Diamond alifanya show huko Dar Live na baada ya kumaliza aliondoka haraka na kwenda Next Door na kuruka na Davido kwenye ‘My Number One Remix’ huku shangwe likiwa kubwa kwa mashabiki waliojazana hapo.

Baada ya kumaliza show hiyo ya kama dakika 8 hivi, Diamond alisikika akisema kuwa “Nimekuja kumpasupport rafiki yangu tukutane Wasafi Festival,” amesema.

Baada ya maneno hayo alitoka jukwaani na kuondoka akiwaacha watu wakipiga shangwe kubwa sana.

Mrejesho toka kwa mashabiki

Nao clouds wameposti picha katika ukurasa wao wa Instagram wakimtag Diamond wakisema kuwa amefika Nextdoor kumpasuport mshikaji wake.

Hizo comments chini sasa moja ya mtu maarufu mtandaoni anayefahamika kwa jina la Hasmovich yeye amesema hivi

“Support hiyo si angemsubiri nje ya ukumbi, kupenda kiki kajikuta yuko mikononi mwa Clouds shikamoo Kusaga,” amemalizia hivyo.

Mwingine amekuja kuomba Clouds na Diamond wakae na wayamalize ili sanaa iende vizuri.

Mwingine ameponda kwanini amekuja kujipendekeza, ameamua kujirudisha mwenyewe.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.