banner68
banner58

Mbasha atoa ufafanuzi juu ya kumpenda Jokate

Mbasha ambaye aliachana na aliyekuwa mke wa Frola Mbasha kwa sasa hana mke

Mbasha atoa ufafanuzi juu ya kumpenda Jokate

Mbasha ambaye aliachana na aliyekuwa mke wa Frola Mbasha kwa sasa hana mke

16 May 2018 Wednesday 13:10
Mbasha atoa ufafanuzi juu ya kumpenda Jokate

Na Amini Nyaungo

Msanii wa nyimbo za injili Emanuel Mbasha amesema kuwa anampenda Jokate kwa nyanja zote.

Swali hilo limekuja mara baada ya kuweka picha katika ukurasa wake wa Instagram ikimueleza kuwa ipo siku ndoa yao itafika na kila kituo cha televisheni nchini itaonesha sherehe yao.

Wengi walitafsiri mengi sana hasa baada ya aliyekuwa anahisiwa kuwa mpenzi wake Ali Kiba kuoa.

Mbasha amesema anampenda kwa aina zote na anajua namna gani anampenda.

“Jokate nampenda, anajua namna gani nampenda, nampenda kama dada, nampenda kama mtumishi unajua tena,” amesema.

Pia ametoa ufafanuzi juu ya kupiga picha na magari wengi wanamsema kuwa sio yake.

“Magari yote yangu hakuna gari la mtu, yapo mawili hivyo watu waelewe hivyo, mimi mfanyabiashara, naimba gospel,” aliandika.

Mbasha ambaye aliachana na aliyekuwa mke wa Frola Mbasha kwa sasa hana mke.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.