banner68
banner58

Mchungaji Lusekelo anena kuhusu Ali Kiba na Diamond

Mchungaji Lusekelo anena kuhusu Ali Kiba na Diamond

24 May 2018 Thursday 11:40
Mchungaji Lusekelo anena kuhusu Ali Kiba na Diamond

Na Amini Nyaungo

Mchungaji wa Kanisa la upako Tanzania, Anthony Lusekelo amewatofautisha Diamond na Ali Kiba kwa kile alichokiiona katika maisha yao ya kawaida.

Mchungaji huyo mwenye makazi yake  ubungo Dar es Salaam amesema anampenda Diamond kwakuwa mtu mnyenyekevu hana maringo kama alivyo mkali mwenzake Ali Kiba ambaye amemtafsiri kama mtu mwenye maringo .

"Mimi nampenda sana Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu, Simpendi Alikiba kwa sababu ana kiburi, nadhani kwa sababu amekaa Kariakoo. Ukipigia simu Diamond anapokea kwa unyenyekevu ila Alikiba anapokea kwa maringo. Ndo maana Diamond amefika mbali," Amesema.

Ameyasema hayo asubuhi akiwa na Times FM katika mahojiano na kituo hiko ambapo baada ya kauli hiyo imeleta tafsiri nyingine kwa mashabiki mara baada ya Times FM kuweka maelezo hayo kupitia ukurasa wao wa instagram.

Maoni ya mashabiki wengi wakiwa wanamshauri mtumishi huyo kuwa maswala ya ushabiki awaachie wao yeye amtumikie Mungu katika kuwapa maneno yake sio kuingia katika katika mjadala isiyomuhusu, ukizingatia mambi ya muziki wa kidunia.

Wengine wamefika mbali na kusena biashara anayofanya mchungaji huyo ndio anayofanya Diamond hivyo lazima ampende mshirika wake. Wengine wamekwa wakimuunga mkono kuwa yupo sahihi Ali Kiba analinga.

Je ni sahihi watu walionahadhi ya muonekano wa kiimani kuingia katika mijadala ya wasanii ambao wanapendwa zaidi huku akionekana kumsifia mmoja, ungana mjadala huu katika ukurasa wetu wa facebook andika azaniapost pia Twitter na Instagram.

Azania Post

Updated: 24.05.2018 11:58
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
jakobo yohana 2018-05-26 16:13:38

sikweli binafsi naamini kua Ali kiba nimtu wawatu mnyekevu anamuonekano namaadiri mema kwajamii ila daimond na lusokelo wate wafanya biashara halam frimason ndimana wanapeana sapoti sikuhizi hakuna dini bwana niuchawi mtupu