banner58

Mpoto achochea bifu la Ali Kiba na Diamond

Mpoto achochea bifu la Ali Kiba na Diamond

29 May 2018 Tuesday 14:44
Mpoto achochea bifu la Ali Kiba na Diamond

Mwanamuziki wa nyimbo za asili nchini, Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba ambaye kwa sasa anatamba na kibao cha ‘Nimwage Radhi’ alichofanya na msanii toka kundi la WCB, Harmonize amesema anatamani uhasama uliopo kati ya Diamond Platinumz na Ali Kiba uendelee kuwepo daima.

Mpoto amesema uhasama wao umekuwa na manufaa katika muziki wa Bongo Flava na burudani kwa ujumla na kwamba anaona wakipatana watapoteza ladha ya muziki huo wa Tanzania unaokuja juu.

”Yaani mwenzenu hilo bifu la Diamond na Kiba nalifurahia sana, limeleta utamu katika muziki ninachoomba tu libaki katika soko la muziki na lisiwe lile la kushindwa hata kusalimiana” amesema Mpoto.

Mpaka leo naamini wanaowatengenezea uadui ni mashabiki wa muziki wao kitu ambacho ni kizuri kinachowasaidia katika muziki wao.

Mpoto ameongezea kuwa haoni sababu ya wawili hao kutoa nyimbo pamoja kwa kuwa wataharibu utamu mzima na ushindani wao na kutaka wabaki hivyo hivyo.

Toa maoni yako juu ya mtazamo wa Mrisho Mpoto wako.

Dar24

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.