Mr Blue amtolea neno Diamond Platnumz

Herry Samir ama jina la usanii Mr. Blue amekanusha kuwa bifu na mashabiki juu ya Diamond Platnumz

Mr Blue amtolea neno Diamond Platnumz

Herry Samir ama jina la usanii Mr. Blue amekanusha kuwa bifu na mashabiki juu ya Diamond Platnumz

05 June 2018 Tuesday 12:26
Mr Blue amtolea neno Diamond Platnumz

Na Amini Nyaungo

Msanii wa Hip Hop Tanzania Mr Blue amewambia mashabiki wake kuwa hana bifu na Diamond Platnumz kama watu wengi wanavyodhani.

Herry Samir ama jina la usanii Mr. Blue amekanusha kuwa bifu na mashabiki juu ya Diamond Platnumz moja ya wasanii waliofanikiwa katika soko la muziki Tanzania.

Blue ambaye ni baba wa watoto wawili amewaambia waandishi wa habari kuwa hana ugomvi na msanii huyo, huku akiweka wazi kwamba yeye ni miongoni wa mwa watu waliowahi kumpa ‘tafu’ Diamond tangu akiwa hafahamiki na waandishi wa habari.

“Mimi ni miongoni mwa wasanii niliowahi kumsaidia Diamond katika muziki wake tena kabla hata waandishi bado hawajamjua,” alisema Blue.

“Ukikaa na Diamond ukimuuliza atakujibu kwamba mimi nilimsaidia tangu awali, alinifuata kama brother wake nikamsaidia kwenye muziki,” amesema.

Diamond na Mr. Blue waliwahi kufanya ngoma ya pamoja ambapo humo ndani msanii huyo aliwahi kuchana kama mwana ‘Hip Hop’.

Ngoma yenyewe inaitwa ‘Jisachi’ ambayo amefanya na hayati Ngweah.

Hivi karibuni baada ya Diamond kutoa ngoma yake ya ‘Iyena’ Mr Blue ameiposti kupitia katika ukurasa wake wa Instagram ndipo maswali mengi yakaanza kuulizwa kupitia hapo, huku wengi wakifikiri Mr Blue yupo karibu na Ali Kiba.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
julys ayagirwe julien 2018-06-15 16:10:56

Mr. blue King Of Hip Pop