banner68
banner58

Mtandao upi hutumika zaidi Tanzania, wamiliki wa ‘Apps’ wanatengeneza vipi pesa?

Mtandao upi hutumika Zaidi Tanzania na ulianza mwaka gani?

Mtandao upi hutumika zaidi Tanzania, wamiliki wa ‘Apps’ wanatengeneza vipi pesa?

Mtandao upi hutumika Zaidi Tanzania na ulianza mwaka gani?

17 May 2018 Thursday 17:20
Mtandao upi hutumika zaidi Tanzania, wamiliki wa ‘Apps’ wanatengeneza vipi pesa?

Na Amini Nyaungo

Watanzania wamekuwa watumiaji wazuri wa mitandao ya kijamii haswa, Facebook, Instagram na Twitter, zaidi ya watumiaji milioni 23 wanatumia huduma hiyo kwa ripoti iliyotoka mitandaoni mwaka uliopita.

Idadi hiyo inatoa utofauti kabisa ya miaka ya nyuma kwani miaka 6 iliyopita ilikuwa watumiaji milioni 7 pekee.

Wakati mwaka 1993 ilikuwa huduma hii ya Internet kwa hapa Tanzania ilikuwa asilimia moja pekee hivyo ni utofauti mkubwa sana sasa.

Kwa mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika sana iwe kwa faida au wengine kwa uharifu japo tayari kwa sasa idara ya Mawasiliano (TCRA) imefanikiwa kudhibiti kwa kiasai kikubwa.

Tanzania ina Zaidi ya wakazi milioni 55 na inasemekana zaidi ya watu milioni 25 wanatumia simu zenye huduma ya Internet.

Mtandao upi hutumika Zaidi Tanzania na ulianza mwaka gani?

Facebook

Mtandao huu umefanya vizuri sana Tanzania. Ulianzishwa February 4, 2004; ni miaka 14 sasa imepita.

Umetumika sana japo umepungua kasi baada ya kufahamika kwa mitandao mingine kwa hapa Tanzania.

Hii inatokana na kubadilisha mara kwa mara kwa muonekano wa ukurasa huo huku ikiwa na huduma ya kutuma ujumbe inayoitwa `Massanger` ambapo unaweza kupiga simu kwa sauti na video.

Mmiliki wa ukurasa huu anaitwa Mark Zuckerberg ameona aongeze Whatsap na Instagram kwa kuinunua japo hajaanzisha yeye, Messenger na Oculus VR.

Facebook inatumika sana haswa ukiwa na simu yenye uwezo wa kutumia Internet unaweza kufungua ukurasa huo na kuanza kutumia.

Watumiaji zaidi ya billion 2.2 kwa mwezi kwa ripoti iliyotoka mwezi January.

Makao makuu yake yapo Menlo Park, California, nchini Marekani.

Instagram

Hii ndio habari ya mjini kwa hivi sasa ambapo mtu mwenye wafuasi wengi Zaidi hapa Tanzania ni Diamond Platnunz, akiwa na wafuasi milioni 4.7 na ndiye wa kwanza kufikisha wafuasi `followers` milioni moja.

Ukurasa huu ulianzishwa October 6, 2010 miaka 7 tayari imepita hadi sasa lakini inawatumiaji zaidi ya milioni 800 kwa mwezi.

Wengi wanaita mtandao wa vijana haswa kwa aina ya picha wanazotumia lakini pia waandishi wa habari wanapata habari kupitia mtandao huo haswa kulingana na namna wanavyotuma picha na vipande vya dakika moja vya sauti.

Mtandao huu umekuwa mzuri haswa hauna mambo mengi kwani kazi yao kupiga picha kali kuziweka katika muonekano mzuri wanazituma huku wengine wenye wafuasi wengi wanapata matangazo.

Inatumika kwa lugha 36.

Twitter

Huu una miaka 12 sasa tangu uanzishwe, inaonekana wanasiasa, wasomi na watu wenye nyadhifa kubwa mbalimbali ndio hutumia mtandao huo.

Vijana wengi hawaupendi kutokana na matumizi yake na ukweli kwamba, chochote kinachowekwa, au kupostiwa kusogezwa chini haraka.

Ina utajiri usipungua US$ -108.06 million ripoti iliyotolewa mwaka 2017, watumiaji zaidi ya milioni 330.

Je wewe ulianza kutumia mitandao ya kijamii mwaka gani na upi unaupenda?

Wengi wanajiuliza wamiliki wa `Application` maariufu kama `Apps` mfano Azania Post Apps, Facebook au Instagram na nyingine nyingi.

Matangazo ndiyo huwanufanisha wamiliki wa apps hizo.

Azania Post

Updated: 17.05.2018 17:35
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.