Nandy bwana ajipa mtihani na kujisahihishia mwenyewe

Kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Ninogeshe

Nandy bwana ajipa mtihani na kujisahihishia mwenyewe

Kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Ninogeshe

15 June 2018 Friday 11:18
Nandy bwana ajipa mtihani na kujisahihishia mwenyewe

Na Mwandishi Wetu

MWANAMUZIKI wa Bongo Flava ajulikanaye kwa jina la Nandera Charles Mfinanga au maarufu kama Nandy amesema kuwa kwa sasa yeye ni bora kuliko wenzake wote wa kike nchini Tanzania.

Nandy ambaye anajitapa kuwa yeye ni malkia wa Afrika anasema kuwa kwa sasa yeye ni zaidi ya wenzake kama Lady Jay Dee na Vanesa Mdee.

Kwa mujibu wa Nandy ambaye wimbo wake mpya wa ‘Ninogeshe’ unafanya vizuri sokoni, idadi ya mashabiki wanaotembelea kwenye mitandao mbali mbali imekuwa ikiongezeka kwa kasi kubwa.

“Mwanamuzi bora wa kike wa Bongo Flava kwa sasa hapa Tanzania ni mimi, unafikiri nani? Nenda Youtube, na sehemu mbali mbali, alisema katika mahojiano na runinga mmoja nchini.

Hata hivyo Nandy alifafanua kuwa kabla ya kuwa nambari one, alimtambua LadyJay dee kuwa zaidi na aliheshimu sana kazi zake kwa sababu aliwajengea msingi mzuri sana kwa wao kufanikiwa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.