Nandy kufanya ngoma na Rihanna

Anatarajiwa kufanya kazi na wasanii wengine wakubwa kama Yemi Alade na Wizkid kutoka nchini Nigeria

Nandy kufanya ngoma na Rihanna

Anatarajiwa kufanya kazi na wasanii wengine wakubwa kama Yemi Alade na Wizkid kutoka nchini Nigeria

30 May 2018 Wednesday 14:40
Nandy kufanya ngoma na Rihanna

Na Amini Nyaungo

Bongo Flava inazidi kung'ara kimataifa baada ya msanii wa kike nchini Nandy kupokelewa kimalkia huko Kenya, huku akitaja baadhi ya 'Collabo' kubwa atakazozifanya siku za usoni.

Nandy ambaye anafanya vizuri katika radio na vituo vya runinga hapa Tanzania na nje ya nchi ameiambia Radio Hot90 FM ya Kenya kuwa anakazi amefanya na Mnigeria Yemi Alade huku zikisalia za Wizkid na Rihanna.

Hii imekuja baada ya kuulizwa atafanya kazi na msanii yupi mkubwa.

"Wapo kama watatu Yemi Alade tayari tumeifanya, kuna Wizkid na Rihanna," amesema.

Wakati huo huo Msanii huyo amesema anatamani aolewe na apate watoto mapacha.

Nandy ana ngoma ambazo zinafanya vizuri, ikiwemo 'Ninogeshe' ambayo ndo inayotamba sasa hivi, nyingine ile ya 'Kivuruge' pamoja na 'Nagusagusa'.

Azania Post

Keywords:
RihannaNandy
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.