banner68
banner58

Rich Mavoko aishinda WCB, ang’atuka rasmi

Rich Mavoko aishinda WCB, ang’atuka rasmi

09 August 2018 Thursday 14:34
Rich Mavoko aishinda WCB, ang’atuka rasmi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko ameripotiwa kushinda kesi dhidi ya Label yake ya zamani WCB na kufanikiwa kuvunja mkataba na kutoka.

Rich Mavoko ambaye alijizolea umaarufu miaka ya nyuma kwa vibao vyake vikali  alisainiwa na kujiunga na WCB siku za nyuma kidogo na kutoa nyimbo kadhaa zilizomrudisha Kwenye chati.

Lakini mapema mwaka huu kulikuwa na tetesi nyingi baada ya Rich Mavoko kutoonekana Kwenye shughuli mbali mbali za WCB na hata kutoonekana kwenye trailer ya shoo mpya ya Wasafi.

Rich Mavoko pamoja na uongozi wake WCB wamekuwa kimya juu ya Tetesi za Rich Mavoko kuondoka WCB Mpaka sasa ambapo kuna taarifa kuwa Mavoko kajitoa rasmi.

Kituo cha Televisheni cha TV E  wameripoti kuwa siku ya leo Mavoko amefanikiwa kushinda kesi dhidi ya WCB rasmi na inasemekana amejitoa Kwenye Label hiyo Lakini pia mkataba alikuwa nao umevunjwa.

Mpaka hivi sasa Rich Mavoko hajatoa tamko lolote kuhusu  nini kinachoendelea Mpaka sasa uongozi wa WCB haujatoa tamko juu ya tuhuma hizo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.