banner58

Rosa Ree awafundisha Diamond, Ali Kiba na Vanessa Mdee namna ya kusaini mkaba mnono

Rosa Ree awafundisha Diamond, Ali Kiba na Vanessa Mdee namna ya kusaini mkaba mnono

30 May 2018 Wednesday 13:54
Rosa Ree awafundisha Diamond, Ali Kiba na Vanessa Mdee namna ya kusaini mkaba mnono

Na Amini Nyaungo

Mkataba mnono alioingia rapa wa kike kutoka Tanzania Rosa Ree hivi karibuni unatarajiwa kubadili kabisa maisha yake.

Rosa Ree amepata menejimenti mpya kutoka nchini Afrika Kusini, inayofahamika kama Dimo Production hivyo kuingia nayo mkataba wa miaka mitatu ambapo kwa kipindi chote hicho watakuwa wakisamamia kazi zake za kisanii.

Pia menejimenti hiyo imemkabidhi Rosa Ree nyumba yenye dhamani ya zaidi ya Milioni 400 na nyingine ipo Afrika Kusini.

Wimbo mpya wa Rosa Ree ‘Way Up’ ambao amemshirikisha rapper Emtee kutoka Afrika Kusini ndio wa kwanza kutoka baada ya kuwa chini ya menejimenti hiyo.

Aina ya mkataba wake ni kama funzo kwa wasanii wakubwa nchini Ali Kiba, Diamond Platnumz, na Vanessa Mdee ambao wamesaini mikataba katika ‘label’ kubwa ulimwenguni japokuwa haijafahamika undani juu ya mikataba hiyo na wanafaidika kwa kiasi gani.

Wasanii hao Ali Kiba (Sony Music Entertainment ya Marekani), Diamond Platnumz na Vanessa Mdee (Universal Global Music pia ya Marekani).

Rosa Ree atakuwa anaikumbuka ‘management’ yake ya awali ya ‘The Industry’ inayosimamiwa na Nahreel ambaye ndiyo amemfungulia milango baada ya kuona kiwango chake.

Aina ya mikataba kama hii ndio mara ya kwanza kupatikana kwa wasanii wa kike katika Rap hapa Tanzania huku akiwa miongoni mwa wasanii wanne waliopata mikataba minono.

Rapa huyo amefanya vizuri tangu aachane na uongozi wake wa zamani miezi saba iliyopita na hatimaye neema imekuja kwake.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.