Sam Wa Ukweli afaraki dunia, Diamond amlilia 

Babu Ally amesema ni moja ya wasanii waliokuwa wanauwezo mkubwa sana japo hapo kati alinyamaza kidogo, aliwahi kushiriki mengi wakati anafanya harakati za....

Sam Wa Ukweli afaraki dunia, Diamond amlilia 

Babu Ally amesema ni moja ya wasanii waliokuwa wanauwezo mkubwa sana japo hapo kati alinyamaza kidogo, aliwahi kushiriki mengi wakati anafanya harakati za....

07 June 2018 Thursday 10:10
Sam Wa Ukweli afaraki dunia, Diamond amlilia 

Na Amini Nyaungo

MASTAA wamlalilia `Sam Wa Ukweli` baada ya kufariki hapo jana, Diamond ni mmoja ya watu walionesha kuomboleza msiba wa msanii huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram akiweka mshumaa.

Diamond ameandika kuwa `mbele yako nyuma yetu Sam, Ins Sha Allah Mungu ailaze roho yako na wote waliotangulia mahala pema peponi Aamin, ``.

Diamond aliwahi kuimba nyimbo na msanii huyo aliwahi kuimba nyimbo moja ambayo wameshirikishwa na Top C inayoitwa `Usiniumize roho` mwaka 2009.

Sam wa Ukweli kwa taarifa iliyotoka kwa rafiki zake wa karibu aliwaambia kuwa hali yake sio nzuri wakiwa studio kuwa anaumwa sana na hatimaye jana amepoteza maisha.

Nyimbo ambayo imemtoa msanii huyo ambapo zamani alikuwa anakaa Kiwalani ni ile ya `Sina Raha` baadaye ametoa nyimbo kali kama vile `Hata kwetu wapo` aliyomshirikisha Salu B.

Azania post imefanya mahojiano na moja ya watu wakaribu alipowahi kuishi Kiwalani.

Babu Ally amesema ni moja ya wasanii waliokuwa wanauwezo mkubwa sana japo hapo kati alinyamaza kidogo, aliwahi kushiriki mengi wakati anafanya harakati za kutoka.

``Jamaa alikuwa mpole sana, na mchapa kazi, nakumbuka ngoma yake ya kwanza sina raha tulifanya mengi sana ila ndio ahadi yake imefikia, ``amesema.

Said Mpapuka `Sasham` yeye ni moja ywatu waliowahi kukaa naye huku amesema hakuwa na ttabu hata wakati anafanikiwa kutoka alikuwa hajabadilika.

Huku Mastaa wengine wakiandika nakuonesha majonzi yao juu ya msanii huyo ambaye aliofanya ngoma zenye hisia sana.

Azania post tunawaombea wote waliotangulia Munghu azilaze roho zao mahali pema peponi Aamin.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
ALEXIX ONEXMUX WABULULU 2018-06-09 16:12:50

We loved you sam but God loved you most rest in peace bro...we xhall miss u alot... amen