Sijawahi kuachwa Mimi ndio naacha - Mama Diamond Platnumz

Adai yeye ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho juu ya ndoa ya mwanae Diamond

Sijawahi kuachwa Mimi ndio naacha - Mama Diamond Platnumz

Adai yeye ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho juu ya ndoa ya mwanae Diamond

14 June 2018 Thursday 13:15
Sijawahi kuachwa Mimi ndio naacha - Mama Diamond Platnumz

Na Mwandishi Wetu

Mama wa mwanamuziki staa Tanzania Diamond Platnumz, ameweka wazi kuwa hajawahi kuachwa katika mahusiano ya mapenzi, ila yeye ndio huwaacha wanaume.

Hii imekuja baada ya kuposti picha yake katika ukura wa Instagram akisema kuwa yeye ndiyo muamuzi mkuu kwa mwanae endapo anataka kuoa.

"Kiuhalisia mimi ndio final say subirini Reality show kupitia wasafi TV," ameandika.

Baada ya hapo ndipo shabiki wake mmoja aliyefahamika kwa jina la Sharifatracey2017, alipohoji kuwa ''hiyo final say yako ndio maana mumeo alikuacha, maana unakiuka hata vitabu vya dini.''

Ndipo alipomjibu kuwa, "Sijawahi kuachwa mpendwa wangu, labda mimi ndio naacha, waulize wanaonijua toka usichana wangu sipelekeshwagi,'' ameandika.

Hii anamaanisha uvumi wa nani amuoe, Hamisa Mobeto, Wema Sepetu au Zari Hassani, yeye ndio ataamua nani amuoe.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.