Trey Songz kuburuzwa mahakamani

Polisi na mpiga picha ambao walikuwepo eneo la tukio wamedai kuwa waliumia

Trey Songz kuburuzwa mahakamani

Polisi na mpiga picha ambao walikuwepo eneo la tukio wamedai kuwa waliumia

06 June 2018 Wednesday 17:18
Trey Songz kuburuzwa mahakamani

Trey Songz ameburuzwa tena mahakamani na wahanga wa vurugu alizozifanya kwenye show ya Detroit mwaka 2016.

Kwenye hiyo show Trey Songz alikasirika na kuanza kuvunja na kurusha vitu stejini baada ya kuzimiwa mic kwa sababu alizidisha muda.

Polisi na mpiga picha ambao walikuwepo eneo la tukio wamedai kuwa waliumia wakati Trey anafanya vurugu jukwaani, wakili wao amedai kuwa wanaweza kutaka mamillion ya Pesa kuimaliza kesi.

Imedaiwa polisi huyo aliumia na hawezi tena kufanya kazi ya upolisi kwa sababu ya Trey, huku mpiga picha naye anadai kuwa alipigwa na mic kichwani.

Trey Songz alikuwa ameshakubali makosa mawili ikiwemo la kuvuruga amani na kuhukumiwa miezi 18 ya kuwa chini ya uangalizi (probation).

Azania Post

Keywords:
Trey Songz
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.