Uongozi wa WCB kumgeuzia kibao Queen Darleen

Kuongeza msanii mwingine maarufu wa kike kwenye lebo ya Wasafi Classic

Uongozi wa WCB kumgeuzia kibao Queen Darleen

Kuongeza msanii mwingine maarufu wa kike kwenye lebo ya Wasafi Classic

21 June 2018 Thursday 16:11
Uongozi wa WCB kumgeuzia kibao Queen Darleen

Na Amini Nyaungo

Maswali mengi yameulizwa kwa nini label inayofanya vizuri ya Wasafi Classic Baby(WCB) ina msanii mmoja wa kike.

Majibu ya maswali hayo anayo meneja wa Diamond, Babu Tale ambaye amethibtisha kuwa watamtambulisha msanii mpya wa kike muda si mrefu.

Imekuwa muda mrefu sasa dada yake Diamond Queen Darleen kuwa mwanamke pekee aliye katika labo hiyo.

Babu Tale amesema labo hiyo itaongeza msanii wa kike muda si mrefu na msanii anayefahamika hivyo wapenzi na mashabiki wa labo hiyo wakae mkao wa kula.

“So tutaongeza haya ni maoni yenu ambayo mmekuwa mkitusapoti, tutakuja kuongeza msanii wa kike ambaye tunajua mtamfurahi wote,” amesema Babu Tale.

Kwa kipindi alichokuwa WCB, Queen Darleen ameweza kuachia ngoma kama Kijuso, Ntakufilisi, Touch na kushiriki kwenye wimbo ‘Zilipendwa’ ambao uliwakutanisha wasanii wote wa label hiyo.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.