Video: Navy Kenzo kutoa dili zito kwa mashabiki wao

Waja na video ya wimbo wao mpya, itazame hapa

Video: Navy Kenzo kutoa dili zito kwa mashabiki wao

Waja na video ya wimbo wao mpya, itazame hapa

14 June 2018 Thursday 13:57
Video: Navy Kenzo kutoa dili zito kwa mashabiki wao

Na Aini Nyaungo

Wasanii wamekuwa wakitumia njia zao kuweza kuufanya wimbo wao kuwa katika masikio ya watu kwa muda wote wanapotoa ngoma.

Kumekuwa na mtiririko mkubwa wa ngoma ambazo nyingine huwa zinashindwa kufanya vizuri kutokana na kutokuwa na ubora unaotarajiwa na mashabiki.

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu ili kumlea mtoto wao wa kwanza Nahreel na Aika ambao wanaunda kundi la Navy Kenzo wametoa dili kwa mashabiki zao kwa kipindi hiki kigumu.

Kundi hilo linawaalika wote ambao wanaweza kucheza vizuri ngoma yao ya `Fella` ambayo imetoka hivi karibuni na tayari ina watazamaji 120,881 kwenye YouTube.

Shabiki atakayeonesha uwezo wa kucheza vizuri ngoma hiyo atazawadiwa kiasi cha milioni 2 za Kitanzania.

Hii imekuwa motisha na shukrani kwa muda wote ambao walikuwa wanasubiria kazi zao.

Azania Post

Updated: 14.06.2018 14:07
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.