Wema amekataa tamaa juu ya Diamond

Maneno yake yanaashiria kuchoka kuhisiwa kuwa huenda akaja kuwa mke wa msanii huyo maarufu wa Bongo Flava

Wema amekataa tamaa juu ya Diamond

Maneno yake yanaashiria kuchoka kuhisiwa kuwa huenda akaja kuwa mke wa msanii huyo maarufu wa Bongo Flava

02 June 2018 Saturday 11:38
Wema amekataa tamaa juu ya Diamond

Na Amini Nyaungo

Wakati Babu Tale akielekea Afrika Kusini kusuluhisha penzi la Diamond na Zari, muigizaji maarufu Tanzania anayefahamika kama ‘Tanzania Sweetheart,’ Wema Sepetu anataka Diamond aoe kweli isiishie katika video.

Wema aliandika ijumaa kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa anatamani mpenzi wake huyo wa zamani afunge ndoa ili waje kula ubwabwa huku wakicheza ngoma yake mpya ya ‘Iyena aliyomshirikisha RayVanny.

Maneno yake yanaashiria kuchoka kuhisiwa kuwa huenda akaja kuwa mke wa msanii huyo maarufu wa Bongo Flava.

New Track Alert Ila kama ingekuwa Pambe ingekuwa Kweli. Just thinking out Loud, Diamond Chibudeeee Fanya kweli bwana. Inshallah mwaka huu hata mwakani. Tuje kucheza Baikoko sie, Rayvanny Kazi nzuri,” aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Huenda maneno ya Wema yanaondoa uvumi kuwa Diamond huenda akarudiana naye na kumuoa.

Upande wa mawifi wa Wema, wanaonekana kumkubali sana Wema huku Esma Platnumz ndiye haswa anaonyesha dhahiri kaka yake amuoe Wema.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.