Wolper amgomea Harmonize, aiita lebo ya Diamond ‘matapeli’

Wolper amgomea Harmonize, aiita lebo ya Diamond ‘matapeli’

06 June 2018 Wednesday 13:22
Wolper amgomea Harmonize, aiita lebo ya Diamond ‘matapeli’

Na Amini Nyaungo

Msanii wa bongo Movie Jackline Wolper maarufu kama ‘Gambe’ ameugomea uongozi wa Wasafi Classic Baby juu ya ushiriki wake kwenye tamasha la Harmonize linalotarajiwa kufanyika siku ya Iddi Pili pale Dar Live, Temeke jijini Dar es Salaam.

Jana Harmonize aliongea na vyombo vya habari kutambulisha tamasha lake ambalo limepewa jina la ‘Kusi Night’ huku akimtaja aliyekuwa mpenzi wake Jackline Wolper kuwa ndiye atakaye simama kama mshereheshaji wa tukio hilo.

Masaa machache baada ya kupata taarifa hizo, akiwa jijini Nairobi, Wolper ametumia ukurasa wake wa Instagram na kusema kuwa hahusiki na tamasha lolote na kwamba waepuke matapeli.

“Naombeni mtambue kuwa sipo Tanzania na sitokuwepo kwenye ‘show’  yoyote, iwe ya Mbagala au Posta, mimi kama Wolper sihusiki, yote mnayoyasikia wanayosema ni uongo wanataka kuwatapeli. Sitaki mtu atumie jina langu kuvuta watu, epuka matapeli,” ameandika.

Muda mchache baada ya posti hiyo, Harmonize ameibuka chini na kuandika `comment` inayoshangaa huku akihoji kuwa inawezekana Instagram hiyo imeibiwa na wadukuzi.

Watanzania kama ilivyo kawaida yao mambo yaliyotofauti ndio wanajazana kuongea posti hiyo imepata `comments` zaidi ya 1500 zikimsifu kwa uthubutu wake wa kuwakatalia wasafi wengine wakimtaka akubali.

Azania Post

Updated: 06.06.2018 14:21
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.