banner68
banner58

Yvonne Chaka Chaka kuja na collabo ya Ali Kiba kesho

Wawili hao walikutana nchini Afrika Kusini wakati Ali Kiba alipokwenda kupokea tuzo yake ya MTV EMA

Yvonne Chaka Chaka kuja na collabo ya Ali Kiba kesho

Wawili hao walikutana nchini Afrika Kusini wakati Ali Kiba alipokwenda kupokea tuzo yake ya MTV EMA

16 May 2018 Wednesday 14:32
Yvonne Chaka Chaka kuja na collabo ya Ali Kiba kesho

Na Amini Nyaungo

Msanii mkongwe kutoka Afrika Kusini Yvonne Chaka Chaka amethibitisha kuwa kesho (Alhamis) watatoa na kuimba kwa pamoja wimbo wake waliorekodi na Ali Kiba.

Baada ya Ali Kiba kutoa singo yake mpya `Mvumo wa radi`, hii inaonekana kukaa vizuri zaidi kwa mashabiki wa Ali Kiba ambao walitamani kuona nyimbo za msanii huyo zikiwa zinatoka mara kwa mara.

Yvonne amesema kuwa anampenda Ali Kiba kwa kuwa anajiheshimu huku akiwa na kipaji cha hali ya juu anamuona kama mwanae.

“Ali Kiba ni kama mwanangu, na yule manager wake Seven Mosha kama mtoto wangu wa kike. Kesho tutaimba kwa pamoja wimbo wetu tulishirikiana ni mzuri sana,” amesema msanii huyo mkongwe barani Afrika na ulimwenguni pia.

Wawili hao walikutana nchini Afrika Kusini wakati Ali Kiba alipokwenda kupokea tuzo yake ya MTV EMA na walipanga wafanye ngoma ya pamoja, hatimaye mwaka ulioisha wamerekodi.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.