Zari ampa njia za mafanikio Diamond

Zari ampa njia za mafanikio Diamond

14 June 2018 Thursday 17:37
Zari ampa njia za mafanikio Diamond

Na Mwandishi wetu

Zari ameonekana kutoa ya moyoni mara baada ya kuona sinema zinazoendelea kwa mchumba wake wa zamani Diamond, akisema kuwa wanafanya kiki zisizokuwa na maana.

Kwa kauli yake inawezekana ikapokelewa vibaya na baadhi ya mashabiki wa mwanamuziki huyo kwa kuwa hawajui undani wa habari hiyo, lakini lengo lake kutaka kuona Diamond akifanya vizuri Zaidi.

Zari ameonekana amechukizwa na kupigwa bumbuazi na kiki pamoja na skendo zinazoendeshwa na Wasafi juu ya `Reality Show` ambayo inatarajiwa kuoneshwa kupitia Tv ya Wasafi.

Zari amesema kuwa haoni sababu ya TV kuendesha vitu visivyo vya msingi katika jamii, akisisitiza kuwa watu wanahitaji kuona vitu vinavyojenga na kupendeza.

Watu wanahitaji kuona michezo, elimu, siasa pamoja na uchumi katika nchi yao pendwa sio mambo yanayoendelea.

“Tv ya kweli inawaletea watu habari za kweli, mfano siasa, uchumi, majumba kuungua na nini kinatokea katika jamii kwa nchi yao,” ameandika.

Amesema kuwa hakuna mdhamini atakayeweza kutoa tangazo kwa TV itakayoonesha vitu visivyo vya msingi.

Ujumbe wake ulikuwa na maelezo mengi ambayo mwisho wa  siku amesema kuwa anataka kuona watu wanafanya mambo makubwa ambayo yana umuhimu katika maisha.

Azania Post

Updated: 14.06.2018 17:39
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.