Zari ataka Diamond kuomba msamaha ili yaishe

Babu Tale afanya sehemu yake, imebaki Chibu kumalizia

Zari ataka Diamond kuomba msamaha ili yaishe

Babu Tale afanya sehemu yake, imebaki Chibu kumalizia

04 June 2018 Monday 12:59
Zari ataka Diamond kuomba msamaha ili yaishe

Na Amini Nyaungo

Waswahili wanasema mjumbe hauwawi, hii inaweza ikawa lugha sahihi kwa meneja wa Diamond anayefahamika kama Babu Tale kuonekana kumaliza kazi ya kusuluhisha mtafaruku baina ya mkali wa Bongo Flava nchini Diamond Platnumz na mrembo wa Uganda Zari.

Hii imekuja baada ya Babu Tale kuposti picha katika ukurasa wake wa Instagram akitanabaisha kuwa ameifanya kazi kwa 50% na zilizobaki 50% ni kwa mkali huyo wa Bongo Flava Diamond kumalizia.

Zari na Diamond, ambao wamepata watoto wawili, waliachana Februari 14 kwa kile Zari alichodai kudharauliwa na msanii huyo katika mahusiano.

Inasemekana Zari anataka Diamond amuombe msamaha ili yaishe baada ya maneno mazuri aliyopataka kutoka kwa Babu Tale na huenda harusi baina ya wawili hao imekaribia endapo 'Chibu Dangote' atakubali kuwa mwanaume wa kweli na kuomba msamaha.

Kupitia BBC Dira ya dunia mrembo Zari alisema wazi kuwa ameachana na Diamond kutokana na tabia zake za kuweka picha akiwa na ex-girlfriend wake.

Wimbo wa 'Iyena' ambao upo kwenye albamu ya Diamond iliyotoka hivi karibuni ya A Boy From Tandale na video yake kuwekwa kwenye mtandao wa YouTube wiki iliyoisha unaonekana kuwa sababu ya Babu Tale kuelekea Afrika Kusini ambako Zari anaishi ili kumaliza tofauti zao.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.