Zari hamkondeshi Diamond ana majanga yake

Yadaiwa ni kazi nyingi ndizo zinazomkondesha

Zari hamkondeshi Diamond ana majanga yake

Yadaiwa ni kazi nyingi ndizo zinazomkondesha

19 June 2018 Tuesday 14:31
Zari hamkondeshi Diamond ana majanga yake

Na Amini Nyaungo

Msanii nyota wa Bongo Flava, Diamond Platinumz amepungua mwili wake wengi walisema huenda kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Zari Hassani imekuwa sababu ya yeye kukonda.

Leo kupitia mkutano na waandishi wa habari meneja wa msanii huyo Babu Tale amesema kazi nyingi ndio zinamkondesha msanii huyo wala sio kitu kingine.

“Diamond anafanya kazi karibu masaa mengi kwa siku, anapigika sana. Sababu kubwa ni hii Wasafi TV mnayoiona. Anaandaa kazi nyingi sana kwa ajiri ya kituo chetu hiki, hivyo sio kitu kingine,” amesema.

Watu kupitia mitandao ya kijamii walimsema sana huku wakihoji kuachana na Zari kunamfanya awe na mawazo mengi hata nuru aliyokuwa nayo siku za nyuma imepotea.

Jibu limepatikana leo kuwa kazi ndi zinamfanya apungue wala sio kitu kingine,” amesema.

Leo amefanya uzinduzi wa Wasafi TV kupitia Startimes channel namba 444.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.