banner68
banner58

Zari na Hamisa wakutana kwa Mwanamitindo

Noel ni maarufu kwa kuwavalisha wasanii wakubwa na watu maarufu

Zari na Hamisa wakutana kwa Mwanamitindo

Noel ni maarufu kwa kuwavalisha wasanii wakubwa na watu maarufu

17 May 2018 Thursday 14:40
Zari na Hamisa wakutana kwa Mwanamitindo

Na Amini Nyaungo

Mwanamitindo na mbunifu maarufu nchini aayefahamika kama Noel amesema haoni tatizo kufanya kazi na Zari Hassani na Hamisa Mobeto.

Noel ambaye ni maarufu kwa kuwavalisha wasanii wakubwa na watu maarufu amesema yeye anaangalia pesa pekee wala sio bifu na mtu.

Ni wazi kwamba Zari na Mabeto wamekuwa na uhasama wa muda mrefu baada ya Hamisa Mabeto kuingilia penzi baina ya ‘Zari The Boss Lady’ na Diamond Platnumz, jambo lililochangia kwa wawili hao kutengana.

Noel amesema anafanya nao wote kazi na wala haangalii ugomvi uliopo baina yao, mradi tu kile anachofanya kinampa fedha.

“Sioni sababu ya kuacha kufanya kazi na watu walio na bifu. Mie nafanya kazi na Zari pamoja na Mobeto wala hakuna tatizo kwani mie nimo katika bifu lao si nafanya kazi tu, mie naangalia pesa,” amesema.

Pia Noel ameongea kwa mara ya kwanza kuhusu kutoonekana kwa muda mrefu kwa mrembo Jokate kuwa ameamua kupumzika kwa muda baadae atarejea na kuweza kuonekana tena.

Azania Post

Updated: 17.05.2018 20:07
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.