Basata wamhoji Steve Nyerere, Irene uwoya

Basata wamhoji Steve Nyerere, Irene uwoya

16 July 2019 Tuesday 15:49
Basata wamhoji Steve Nyerere, Irene uwoya


Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
BARAZA la Sanaa la Taifa(BASATA)  limewahoji wasanii wa filamu nchini, Steve Nyerere na Irene Uwoya kutokana  na tukio la kuwarushia fedha waandishi wa habari.

Vile vile Basata imesema haiwatambui wawili hao kama wasanii kutoka na kutosajiliwa na baraza hilo

Baraza hilo liliwahoji wasanii hao, Julai 17, 2019 jijini Dar es Salaam kufuatia kitendo chao cha kuwarushia fedha Waandishi wa Habari katika kikao chao jana  jana Julai 15

Hata hivyo, Uwoya amewaomba radhi Waandishi kufuatia kitendo hicho kilichopelekea baadhi ya waandishi kuharibu baadhi ya vifaa vyao kutokana na vurugu zilizotokea wakati wa kudaka fedha hizo alizokuwa anarusha

Amesema hakufanya hivyo kwa lengo la kudhalilisha waandishi wa habari kama ambavyo imetafsiriwa na watu wengi, kwani dhahiri anatambua umuhimu mkubwa wa waandishi wa habari katika jamii na kwamba ilikuwa ni furaha kutokana na waandishi kufika kwa wingi

Updated: 19.07.2019 06:40
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.