Beyonce akinadi Kiswahili kimataifa

Beyonce akinadi Kiswahili kimataifa

11 July 2019 Thursday 13:24
Beyonce akinadi Kiswahili kimataifa

HII leo Julai 11, 2019 mwimbaji maarufu nchini Marekani Beyonce ameachia kibao kipya na maneno ya kwanza kabisa ni ya Kiswahili. Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni kuitangaza lugha ya kiswahili dunia kote

"Uishi kwa muda mrefu mfalme," sauti nyembamba inaimba kisha sauti nzito inaitika "uishi kwa", kionjo hiko kinajirudia mara mbili na kisha wimbo kuendelea kwa Kingereza.

Kibao hicho kiitwacho Spirit ni sehemu ya albamu inayosindikiza filamu mpya ya Lion King inayotengenezwa na kampuni kubwa ya Disney ya nchini Marekani.

Mfalme anayeimbwa kwenye kibao hicho ni Simba dume kijana ambaye anaanza safari ya kupambana ili kuwa mfalme wa nyika.

Filamu ya Lion King, "inajumuisha sauti za kutoka barani Afrika," imeeleza kampuni ya Disney.

Kampuni hiyo inasema kuwa albamu hiyo iitwayo The Lion King: The Gift, itaachiliwa ndani ya kipindi cha siku tisa kuendana na uzinduzi wa filamu hiyo duniani kote.

Albamu hiyo imejumuisha vionjo vya waandaa muziki kutoka Afrika, kwa mujibu wa Beyonce ambaye amenukuliwa kwenye taarifa iliyotolewa na Disney.

"Ilikuwa ni muhimu kuwa muziki usiimbwe na wasanii nyota na wenye vipaji bali iandaliwe na waandaaji wa Kiafrika. Ubora na moyo (mapenzi) vilikuwa vitu muhimu kwangu...

"Ni mchanganyiko wa kila kitu, si sauti moja tu. Kuna ushawishi kutoka kila kona, kutoka kwenye R&B, hip-hop na Afro Beat."

Updated: 11.07.2019 13:36
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.