Harmonise afunga ndoa kwa siri

Harmonise afunga ndoa kwa siri

09 September 2019 Monday 06:20
Harmonise afunga ndoa kwa siri

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MSANII wa muziki wa bongo fleva Rajab Abdul Kahali maarufu Harmonize amefunga ndoa na mchumba wake ambaye ni raia wa Italia, Sarah Michelotti siku chache baada ya mwanamuziki huyo kujiondoa rasmi katika kundi la Wasafi Classic Baby WCB ambalo linaongozwa na msanii kinara nchini Tanzania, Diamond Platnums.

Mwanamuziki huyo anayependa kujiita konde boy akimaanisha kuwakilisha wamakonde kutoka kusini mwa Tanzania alimchumbia Sarah miezi michache iliyopita na hakuwahi kutangaza siku rasmi ya harusi yake.

Harusi hiyo ambayo inadaiwa kuwa ya siri ilifanyika jumamosi Septemba 7, 2019 jijini Dar es salaam na kuhudhuria na wageni 100 tu.

Si jambo la kawaida kwa harusi nchini Tanzania kuhudhuriwa na watu wachache kiasi hicho hata kwa watu ambao si maarufu.

Hakuna msanii hata mmoja kutoka kundi lake la zamani la Wasafi aliyeudhuria tafrija hiyo ya mwana muziki huyo.

Pongezi nyingi kwake zimetoka kwa mashabiki na wadau wa tasnia kwa hatua ambayo amepiga na kutajwa kuwa mfano wa kuigwa

Wakati harusi hiyo ikiwashangaza wengi katika mitandao ya kijamii, wengine wakidai kuwa labda ndoa ndio ilikuwa sababu kuu ya mwanamuziki huyo kuacha kuimba na Diamond.

Harmonize kwa sasa anasifika kwa wimbo unaompongeza rais Magufuli katika utendaji wake wa kulijenga taifa unaoitwa 'magufuli'.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.