LHRC wautilia 'shaka' muswada wa sheria ya filamu na michezo ya kuigiza

LHRC wautilia 'shaka' muswada wa sheria ya filamu na michezo ya kuigiza

24 June 2019 Monday 15:53
LHRC wautilia 'shaka' muswada wa sheria ya filamu na michezo ya kuigiza

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
KITUO cha haki na sheria nchini Tanzania (LHRC) kimesema mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ni mapana sana kiasi cha kuweka vikwazo hususani katika maudhui ya picha za video.

Kimesema majukumu ya Bodi ya Filamu (Marekebisho 18)  yanayojumuisha kudhibiti, kufuatilia, kutoa vibali, kuidhinisha na kusimamia ni mapana na  yote hayajafafanuliwa kwa ufasaha.

''Pendekezo la 20 linatoa mamlaka yasiyo ya kawaida ya kudhibiti maudhui, ikisisitiza kwamba kila bango litakaloandaliwa na kubandikwa hadharani linapaswa kupitiwa na kuidhinishwa na Bodi ya Filamu'' inasema taarifa ya LHRC.

LHRC imetoa kauli hiyo kufuatia kuwasilishwa kwa pendekezo la dharura la mswada wa mabadiliko ya sheria Namba 3 wa mwaka 2019 Tanzania unaotoa muongozo wa kazi katika sekta ya filamu.

Mswada huo unapendekeza kufanyika kwa marekebisho ya Sheria ya filamu na michezo ya kuigiza kudhibiti kazi zinazofanyika katika sekta hiyo nchini.

Mswada huo uliowasilishwa mwishoni mwa juma unapendekeza kuwa kampuni au mtu yoyote anayetengeneza filamu makala au matangazo ya biashara kwa kutumia picha za nchini anastahili kuwasilisha kanda zote zilizorekodiwa kwa bodi ya filamu  kabla ya uhariri wowote.

Kadhalika wahusika wanatakiwa kubaini maeneo yote ambayo wamerekodi na hatimaye kuwasilisha nakala ya mwisho ya makala, tangazo au filamu iliyotengenezwa kwa kutumia picha za ndani au kuihusu Tanzania.

Mswada huo ambao ni mjumuiko wa mapendekezo ya maboresho ya sheria mbali mbali, ulibainishwa wiki iliyopita na kuwasilishwa kwa kamati ya bunge ya katiba na sheria kwa hati ya dharura.

Mswada huo unatarajiwa kuwasilishwa bungeni kujadiliwa kabla ya kupitishwa kuwa sheria Juni 27 wiki hii .

Updated: 24.06.2019 15:59
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.