Msanii Davido azidi kung'aa

Msanii Davido azidi kung'aa

25 July 2019 Thursday 15:17
Msanii Davido azidi kung'aa

JARIDA la Instagram Rich List 2019, limetoa orodha ya watu 100 ambao wanaingiza pesa nyingi kupitia matangazo ya biashara wanayopost kwenye kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Instagram.

Kwa ujumla orodha hiyo inaongozwa na Kylie Jenner, Ariana Grande na Cristiano Ronaldo katika nafasi ya tatu.  Watu wengine maarufu waliopo katika list hiyo ni Kim Kardashian, Beyonce, Lionel Messi, Neymar Jr, Justin Bieber, Nick Minaj, David Beckham na Ronaldinho.

Kutokea barani Africa, Davido ndiye amekuwa msanii wa kwanza anayeingiza pesa nyingi kupitia matangazo anayopost Instagramm ambapo amekamata nafasi ya 38.

Davido analipwa Dola 74,000 sawa na Milioni 170 za Tanzania kwa kila tangazo moja. Pia katika orodha hiyo wapo wasanii kama Wizkid kwenye nafasi ya 46, na Tiwa Savage kwenye nafasi ya 48.

Davido ndiye msanii mwenye wafuasi wengi zaidi katika mitandao ya kijamii ya Instagram na Twitter kutokea barani Africa.  Kwasasa Instagram  ana wafuasi Milioni 11 huku Twitter akiwa na Milioni 5.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.