Msanii Hiba Tawaji anogesha filamu mpya ya Aladdin

Msanii Hiba Tawaji anogesha filamu mpya ya Aladdin

25 May 2019 Saturday 11:40
Msanii  Hiba Tawaji anogesha filamu mpya ya Aladdin

SAUTI ya Mwanadada msanii, Hiba Tawaji imechangia kunogesha filamu ya Aladdin iliyochezwa kwa lugha ya kifaransa na mwigizaji mahiri, Guy Ritchies na kuifanya filamu hiyo kuvutia wapenzi wengi wa sanaa ya filamu tongu ilipotolewa kwa mara ya kwanza siku ya jumatano iliyopita Mei 22, 2019

Mwanadada huyo raia wa Lebanon mwenye umri wa miaka 31 amejizolea umaarufu kwa kuigiza jukumu la mwanamke katika baadhi ya nyimbo za Rahbani musicals, chini ya uasisi wa Rais wa Walt Disney wa nchini Ufaransa. Aliimba kwa mara ya kwanza kwenye filamu ya kifaransa ya speechless an Ce Reve bleu ambayo ilipokelewa na mashabiki wengi wa fani hiyo duniani

Filamu ya Aladdin imeakisi maisha wakati wa karne zilizopita katika eneo la Mashariki ya Kati nyakati za usiku. Ni filamu inayoonesha maisha ya mitaani yaliyojaa mazingaombwe na penzi moto moto dhidi ya Malkia wa rebellion Jasmine

Sinema hii imeongozwa na Guy Ritchie mwaka 2019, mchezaji nyota wa filamu za Hoolywood nchini Marekan Will Smith alisifia na kudai ni moja ya vipaji kama ilivyo kwa mwana dada wa Kiingereza Naomi Scott na mwanadada mwingine mwenye urai wa Canada na Misri Mena Massoud

Updated: 03.06.2019 09:46
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.